SOMO: KUZINGATIA. Luka 15:14-18" Alipokuwa amekwisha tumia vyote, njaa kuu iliingia nchi ile, yeye naye akaanza kuhitaji. Akaenda akashikamana na mwenyeji mmoja wa nchi ile, naye alimpeleka shambani kwake kulisha nguruwe. Akawa akitamani kujishibisha kwa maganda waliyokula nguruwe, wala hapana mtu aliyempa kitu. ALIPOZINGATIA MOYONI MWAKE , akasema, Niwatumishi wangapi wa baba yangu wanaokula Chakula na kusaza....." Mwana mpotevu alipozingatia moyoni mwake akafanya maamuzi ya kurudi kwa baba yake. Kuna watu wanasema siwezi kuacha pombe, sigara, uzinzi au uasherati hii ni vita huwezi kuacha kirahisi lazima useme SITAKII. Kuna watu hawawezi kuishi maisha matakatifu kwa sababu ya vitu vya kupewa, wanapenda vitu vitamu, anasema nitaishije nikiacha dhambi?? Hebu amua kutoka hapo uone, MUNGU hatakuacha uaibike. Amua kufanya maamuzi ya hatari ili utoke kwenye hali inayokusumbua. Amua kurudi kwa BABA yako ambaye dunia na vyote viijazavyo ni mali yake, usiendelee kula na nguruwe ...
Posts
Showing posts from January, 2018
- Get link
- X
- Other Apps
SOMO: KUZINGATIA. FAIDA ZA KUZINGATIA. Unapoamua KUZINGATIA moyoni mwako unasababisha TOBA, UPONYAJI na MABADILIKO KATIKA MAISHA yako, pia unasababisha ile hali ya kuwa na kiburi na kujikweza iondoke kwako. Luka 11: 21 " Yule mwana akamwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; sistahili kuitwa mwana wako tena". Kuzingatia kunaondoa mabishano, mashindano na kujihesabia haki na kunaleta USAIDIZI, MSAMAHA, HURUMA, SHANGWE NA KICHEKO. Hali yako ya KUZINGATIA itakuponya na kukurudisha kwenye yale Mungu aliyokukusudia. Mtumishi wa Mungu Mama Eliakunda Mwingira - EFATHA MINISTRY.
- Get link
- X
- Other Apps
SOMO: KUZINGATIA. Luka 15: 11-32" Akasema, mtu mmoja alikuwa na wana wawili, yule mdogo akamwambia babaye, Baba, nipe sehemu ya mali inayo niangukia. Akawagawia vitu vyake.Hata baada ya siku si nyingi, yule mdogo akakusanya vyote, akasafiri kwenda nchi ya mbali, akatapanya mali zake huko kwa maisha ya uasherati........" Mwana mpotevu alipozingatia moyoni mwake akafanya maamuzi ya kurudi kwa Baba yake, alisema ni kweli nimekosea lakini nitarudi. Na wewe leo usikubali kufa dham bini ondoka na urudi kwa Baba yako wa Mbinguni. Inawezekana unaishi na mume wa mtu, leo amua kuachana nae na urudi kama mwana mpotevu. Ondoa ile hali ya kusema nikiondoka watanionaje, au nitaishije? Yesu leo anakwambia rudi ATAKUPOKEA na yuko tayari KUKUSAIDIA. Mwana mpotevu angeendelea kukaa kule angekufa huku anakula na nguruwe, lakini alipoamua kurudi Baba yake alimpokea akamvika vazi bora, njoo kwa Yesu akutue mizigo ya mateso na magonjwa, Mungu ameandaa USAIDIZI atakusaidia. Amua kumsikiliza R...
- Get link
- X
- Other Apps
MKESHA WA UDHIHIRISHO WA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU, EFATHA MINISTRY PRECIOUS CENTER KIBAHA: Nguvu za ROHO MTAKATIFU zinapokuja kwetu, tunafaidiaka na nini.? 1. Katika UWEPO wake Roho Mtakatifu utajua mambo ya sasa na yale yajayo. Yohana 16:13 “Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.” Ukiijua KWELI ya Mungu ndiyo it akufanya uishi, Bwana Yesu akasema huyo Roho atakapokuja atawaingiza katika KWELI; kwa nini katika KWELI? Kwa sababu ndiyo itakayokupa KUISHI. 2. Utajua kuwa una BABA, MWANA na ROHO MTAKATIFU. 3. Utayajua yale mambo ambayo Umekirimiwa na BABA wa Mbinguni. 1 Wakorinto 2:12 “Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.” Mungu kila iitwapo leo ana jambo la kipekee kwa ajili yetu lakini sisi hatujui na ndiyo maana tunakufa maskini. 4. R...
- Get link
- X
- Other Apps
MKESHA WA UDHIHIRISHO WA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU, EFATHA MINISTRY PRECIOUS CENTER KIBAHA; Huu ni mwaka wa nne wa Mtembeo wa Mungu, huu si Mtembeo wa Mwanadamu bali ni wa Mungu kutembea na watu wake wale ambao amewaridhia, hivyo basi huu ni mwaka wa udhihirisho wa Nguvu za Mungu; hutakaa utikiswe na chochote, shetani hatakaa akutishie tena kwa sababu una Nguvu za Mungu. Matendo 1:8 “Lakini mtapokea NGUVU, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa MASHAHIDI wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.” Hii ni Ahadi ya Mungu kwa wale wanao mwamini Yesu Kristo, kama wewe ni mmoja wao Ahadi hii ni yako si ya shangazi yako wala mjomba wako. Wewe unaye mwamini unapewa Ahadi hii ili uwe shahidi wa mambo ya Mungu kupitia Kristo Yesu; hivyo ukiipata NGUVU hiyo unakuwa na uwezo wa kujionyesha wewe ni muwakilishi wa Mungu huku duniani. © MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA.
- Get link
- X
- Other Apps
EMPOWERMENT OVERNIGHT AT PRECIOUS CENTRE KIBAHA (26th JAN, 2018). © APOSTLE & PROPHET JOSEPHAT E. MWINGIRA This is the day that the Lord has prepared for you to have an encounter with HIM. This is the fourth year in our move with God. In this year the devil will no longer torture you nor intimidate you anymore. Acts 1:8 “But ye shall receive power, after that the Holy Ghost is come upon you: and ye shall be witnesses unto me both in Jerusalem, and in all Judaea, and in Samaria, and unto the uttermost part of the earth.” (KJV) When you have the POWER of God, you have all the ability to show yourself that you are the REPRESENTATIVE of God here on earth. WHAT DO WE GAIN WHEN THE POWER OF THE HOLY SPIRIT COMES? 1. In the presence of the Holy Spirit you will know the reality about things. About the present things and those of the future. "So, you will never be blind." John 16:13 “Howbeit when he, the Spirit of truth, is come, he will guide you into all truth: for h...
- Get link
- X
- Other Apps
MKESHA WA UDHIHIRISHO WA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU, EFATHA MINISTRY PRECIOUS CENTER KIBAHA, Luka15:17 “Akawa akitamani kujishibisha kwa maganda waliyokula nguruwe, wala hapana mtu aliyempa kitu. Alipozingatia moyoni mwake, alisema, Ni watumishi wangapi wa baba yangu wanaokula chakula na kusaza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa.” Mwana mpotevu alipata nafasi kwa Baba yake lakini akaichezea, ndiyo maana baada ya kuipoteza akajuta na kukumbuka nyumbani kwa baba yake, alijua kuwa ny umbani kwao kuna kila kitu ndiyo maana akaamua kurudi kwa Baba yake. Vivyo hivyo ndivyo ilivyo Nyumbani mwa BABA yako wa Mbinguni, kuna chakula cha kutosha; rudi nyumbani kwa BABA yako ili uweze kupokea chakula kutoka kwake maana kwake kuna kila kitu unacho kitaka, ikiwemo Karama na Vipawa vya Roho Mtakatifu na chochote kile unacho kihitaji kinapatikana kwake. © MCHUNGAJI BETSON KIKOTI.
- Get link
- X
- Other Apps
MKESHA MKESHA MKESHA............. MKESHA WA IBADA YA ROHO MTAKATIFU NGUVU YA MUNGU, Leo kuanzia saa mbili usiku Kibaha Precious Centre Efatha Ministry. Mjulishe na mwenzako, na Jirani yako, Ndugu zako, Wazazi wako, Rafiki zako, Wanafunzi wenzio, Wafanyakazi wenzako na Woooooote wenye Mapenzi Mema. Njoo ukutane na NGUVU YA MUNGU, Mkesha wa ROHO MTAKATIFU.
- Get link
- X
- Other Apps
Huduma ya EFATHA MINISTRY inakukaribisha katika MKESHA wa mwisho wa mwezi; "MKESHA WA UDHIHIRISHO WA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU" utakaofanyika PRECIOUS CENTRE KIBAHA siku ya Ijumaa (26/01/2018) kuanzia saa 2 usiku. Mkesha utaongozwa na Mtumishi wa Mungu, MTUME NA NABII JOSEPHAT E. MWINGIRA. Kwa walio mbali, tutaungana kupitia; - Trenet TV. - Youtube (Efatha Ministry). - Facebook page (Efatha Ministry). - Blog (www.efathaministry.blogspot). - Twitter (Efatha Ministry). - Instagram (Efatha Ministry). - Website ( www.efathaministry.org ). - Efatha Radio App (download kupitia playstore). - Mixlr (Efatha Ministry).
- Get link
- X
- Other Apps
SUBJECT: ACCEPT TO BE LED BY THE SPIRIT OF GOD. When we accept to be led by the Spirit of God, we are made the Sons of God. When you accept to be led by His Spirit, the wicked ones will do whatever they can so as to finish you, to make you bankrupt, to shame you, but despite of all those, they won’t succeed because God will cover you. When you accept to be led by the Spirit of God, you will work according to what you have planned and you will have divine POWER within you; bec ause the Son of a King is a King, and that of a lion is a lion. Ecclesiastes 7:25-26 “I applied mine heart to know, and to search, and to seek out wisdom, and the reason of things, and to know the wickedness of folly, even of foolishness and madness: And I find more bitter than death the woman, whose heart is snares and nets, and her hands as bands: whoso pleaseth God shall escape from her; but the sinner shall be taken by her.” (KJV) A SON is not captured by folly things; in Ecclesiastes He said, this i...
- Get link
- X
- Other Apps
SOMO: KUBALI KUONGOZWA NA ROHO WA MUNGU. Tukikubali kuongozwa na Roho wake tunafanyika kuwa Wana wa Mungu. Ukikubali kuongozwa na Roho wa Mungu, wana wa ibilisi watafanya kila wanaloweza ili kukuangamiza, kukufilisi,kukuaibisha, hata hivyo hawata fanikiwa, kwani Mungu atakufunika. Ukikubali kuongozwa na Roho wa Mungu, unafanya kazi kama unavyotaka na unakuwa na NGUVU ya Kiungu ndani yako kwa kuwa Mwana wa Mfalme ni Mfalme na mtoto wa simba ni simba. Mhubiri 7:25-26 "Nikageuka, na moyo wangu ulikazwa katika kujua na kupeleleza, na kuitafuta hekima, na maana ya mambo yaliyoko; ili nifahamu ya kuwa uovu ni upumbavu, na upumbavu ni wazimu......". Mwana hakamatwi na vitu vya kipumbavu, katika Mhubiri akasema, hii ni kama balaa katika nchi; wakuu wakitembea kwa miguu na watumwa wakipanda farasi! Hii ni balaa kubwa! Anamaanisha kuwa, wewe unayeitwa Mtoto wa Mungu umechoka huku wenye dhambi wakiendesha magari ya kifahari. Mbingu na Nchi ni Mali ya BWANA ambaye ni BABA yako; L...
- Get link
- X
- Other Apps
SOMO: TOFAUTI KATI YA MWANA NA MTOTO Yohana1:12" Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio Jina lake". Ni vizuri ukafahamu tofauti ya MWANA na MTOTO na mazingira unayokwenda nayo. Tukimpokea Yesu Kristo; tunaitwa watoto wa Mungu na tukiendelea na WOKOVU, tunaitwa WANA wa Mungu. Watoto ni wale wasioelewa Neno la Mungu kwa kina. Biblia inasema wananyonya maziwa, hawajajua kupambanua Neno bado. Ukiwa mtoto, unarushwa huku na kule, ma ana huna maamuzi, lakini unajengwa utoke kwenye utoto mpaka unafikia ukamilifu kwenye nafasi aliyoko Kristo. Wakamilifu ndio wanaoitwa WANA, ambao wanatenda kile angefanya Bwana Yesu, kama angekuwepo. Hawaitaji aje, bali wao wapo na wanamwakilisha Yesu hapa duniani. Kwa hiyo mtaani kwako ni lazima uonyeshe Bwana Yesu yupo. Waliookoka ni jeshi la Bwana, na wale wachanga ni makuruta ambao hawajafika hatua ya kuwa maafande.Wakishamaliza hiyo hatua ya ukuruta na kufuzu, wanakuwa maafande, napo wanapan...
- Get link
- X
- Other Apps
️MAOMBI NA USHAURI WA MTU MMOJA MMOJA; Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira anawakaribisha watu wote katika USHAURI na MAOMBI ya mtu mmoja mmoja, yanayofanyika kila siku za wiki (Jumatatu hadi Ijumaa) Kanisani Efatha Ministry Mwenge Dar es salaam. JE? NINI KINA KUSUMBUA? NJOO EFATHA MAHALI YESU ANATENDA KAZI.. Kwa msaada zaidi kama unataka Kuokoka, au Maombi wasiliana na Mchungaji kwa No 0754 753 182
- Get link
- X
- Other Apps
SOMO: NGUVU YA MUNGU. Siri ya kupata NGUVU ya Mungu, ni kuishi maisha MATAKATIFU ili ukiomba Mungu apate kukusikia. Umaskini na ufukara ni dalili ya kuwa karibu na shetani kuliko Mungu. Kuipenda dunia na mambo yake, ni kumchukia Mungu na alama ya wazi ni hali ya umaskini. Amua kutafuta haki yake ili mengine uzidishiwe. Hata hivyo hali halisi inaonyesha kuwa, watu wengi wako katika hali ya kukosa na kushindwa; tatizo ni kiwango kidogo cha ujuzi kuhusu makusudi na ahadi za M ungu juu yao na jinsi wanavyo kiri kinyume na mawazo ya Mungu. YEYE anatuwazia mambo mema; hivyo ni lazima kukiri vyema ili kufanya ulimwengu kutimiza kile tunachosema. Suluhisho ni kufanywa upya moyo na fikra, ili zimtii Mungu na Yesu Kristo kwa kuishi maisha MATAKATIFU. : Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira (Efatha Ministry.)
- Get link
- X
- Other Apps
SUBJECT: THE POWER OF GOD. The secret of receiving the POWER of God, is living a HOLY life; so that when you pray, God may listen to you. Poverty and destitution is a sign that you are closer to the devil than with God. The love of the world and its things, is hating God and the easiest symptom of it, is being poor. Desire to seek His RIGHTEOUSNESS so that others may be multiplied unto you. After all the reality of issues reveals that, most people are facing lack and failure; the problem is, "they have little understanding about the purpose of God and His promises upon them and they confess against the thoughts of God. He thinks the best for us; so it's a must that we confess rightly so as to make the world fulfill what we say. The solution is to be renewed, the heart and thoughts so that they may obey God and Jesus Christ; by living a HOLY life. © Apostle & Prophet Josephat E. Mwingira (Efatha Ministry).
- Get link
- X
- Other Apps
THE TIME OF SALVATION IS NOW. # CHANGE . GOD desires that you may hear His voice today. It's possible that you were saved, but you backslide, wake up from where you stumbled; God is full of Mercy, He knows your weaknesses. HE HAS ALREADY FORGIVEN YOU. DECIDE FROM YOUR HEART, IT'S BETTER TO LISTEN TO THE VOICE OF GOD TODAY; BECAUSE YOU WILL NEVER BLAME YOURSELF FOR THIS DECISION. # SHARE
- Get link
- X
- Other Apps
Naibariki Jumatano Yangu (Yako), MUNGU BABA Ni MZURI, YEYE ANANIWAZIA MEMA DAIMA, Mwaka huu AMESEMA Atafanya Chochote ili Mradi niwe na KICHEKO, niwe na FURAHA, niwe na AMANI, Kweli WEWE MUNGU BABA NI MZURI, NAKUPENDA,,,,,,,,,,,,,Jumatano yangu (yako) IMEBARIKIWA. MPENDE MUNGU, MWAMINI MUNGU, ISHI MAISHA MATAKATIFU.
- Get link
- X
- Other Apps
ZONE ZONE ZONE. Zone ni Ibada ya Nyumba kwa Nyumba. Na Ibada hizi za Zone huwa zinafanyika kila siku ya Jumanne.......... ni IBADA KAMILI. Je WEWE Ulikwenda Ibada za Zone katika eneo lako? PICHANI: Ni mojawapo ya Ibada za Zone zilizofanyika leo Duniani kote kwa Wana wa MUNGU Wana EFATHA. Mchungaji Caroline Jonathan akiongoza Ibada latika eneo dogo la Yerusalemu/ Nazareti Ubungo National Housing/ Legho. HONGERA WEWE Uliyekwenda leo Ibadani.
- Get link
- X
- Other Apps
SUBJECT: “THE POWER OF GOD.” The role of this POWER is to posses all the other POWERS that exist, and it can take a person to awesome places. Let no one say that he/she has no POWER, the problem is that they fail to recognize that, which Power is applicable at which point! There is the POWER of God and that of evil, and you cannot recognize the power of evil, if you don’t know the POWER of God. In order for you to know the sweetness of the POWER of God, enter within it; becau se within the POWER of God, there are the seven Spirits and each Spirit has its way of operating. When you were saved, you received POWER; but within that POWER you need FAITH. It was as if you were given the keys that open seven rooms, which are the seven Spirits of God. Within these POWERS you are first of all given the least one so that you may be able to reach the biggest one. The POWER of God takes you from scarcity towards plenty; so you can never be poor, since it does not allow poverty. The POWER of...
- Get link
- X
- Other Apps
SOMO: NGUVU YA MUNGU. NGUVU hii kazi yake ni kumiliki NGUVU zote zilizopo na inaweza kumfikisha mtu mahali pa kushangaza, kwa hiyo mtu asiseme hana NGUVU, tatizo ni kwamba hawezi kubaini NGUVU ipi inatumika wapi. Kuna NGUVU ya Mungu na ya uovu na huwezi kubaini NGUVU ya uovu kama hujaijua NGUVU ya Mungu.Ili uweze kujua uzuri wa NGUVU ya Mungu, ingia ndani maana ndani ya hiyo NGUVU, kuna Roho saba na kila Roho ina namna yake ya kutenda. Ulipookoka ulipata NGUVU, lak ini katika NGUVU hiyo, inahitaji IMANI. Ni kama ulipewa funguo unaofungua vyumba saba, yaani Roho saba za Mungu. Katika NGUVU hizi, unapewa kwanza ndogo ili uweze kufikia NGUVU kubwa. NGUVU ya Mungu inakuhamisha kutoka mahali pa uchache na kukuingiza mahali pa utele kwa hiyo huwezi kuwa maskini maana hairuhusu umaskini. NGUVU ya Mungu inaweza kusababisha utoke kwenye uchungu, ujinga, matatizo na mateso uliyonayo. Mtu hahitaji fedha, bali NGUVU ya Mungu, Maana hiyo ndiyo itakayo sababisha watu wamletee zawadi. Mtumish...
- Get link
- X
- Other Apps
SOMO: KAZI ZA NGUVU YA MUNGU. - Kukamilisha na Kufanikisha Maono ya Kiungu. Yesu alipokuja duniani, alihitaji NGUVU ili kufanikisha Kazi yake. Ili tutoke kwenye misiba na shida tulizonazo, tunahitaji NGUVU ya Mungu. Musa alipowachukua wana wa Israel kutoka Misri kwenda Kaanan, alihitaji NGUVU ya Mungu ili kuwatoa. Kutoka 7:8-13 "BWANA akanena na Musa na Haruni, akawaambia, jifanyieni miujiza; ndipo utakapomwambia Haruni, shika fimbo yako,........" Bila NGUVU za Mungu, Musa asingeweza kuwashinda wale nyoka wa wachawi wa Farao na kuwatoa wana wa Israel Misri. Uzao wa Yakobo waliotoka Misri, ili wamiliki Kaanani, ilibidi watumie NGUVU ya Mungu kupigana na mataifa na ndivyo ilivyo hata sasa. Samsoni aliweza kuua dubu kwa taya la punda kwa NGUVU za Mungu. Waamuzi 14:5-6 "Ndipo Samsoni na baba yake na mama yake wakatelemkia Timna, wakafika mashamba ya mizabibu huko Timna; na tazama, mwana-simba akamngurumia. Roho ya BWANA ikamjilia kwa NGUVU, naye akampasua kana kwamba anampas...
- Get link
- X
- Other Apps
SOMO: USIDHARAU UUMBAJI WA MUNGU. Kila alichoumba MUNGU kinakubalika mbele zake na kina Kusudi maalum kwa ajili yake, tena ni Watumishi wake. Ndani ya hicho kiumbe ameweka hazina ya VIPAWA. Kwa hiyo usimdharau mtu kwa kuwa hujajua bado kesho atakuwa nani? au ana nini kitakachokusaidia au kukuokoa wakati wa uhitaji wako? Tamani wengine wafikie Kusudi la Mungu katika Maisha yao kwa kuwasogeza karibu na Bwana. Chochote ambacho Mungu amekiweka mkononi au mbele yako, pokea na kitunze kwa shukurani kwa kuwa Kazi ya Mungu haina makosa. Katika Biblia Nabii Balam aliokolewa na punda ambaye alimwona Malaika aliyetaka kumuua; Lakini yeye (Balam) hakumuona. Mungu anaweza kutumia kitu chochote ili kutimiza Mapenzi yake, maana anajua kila kinachotokea. Mhubiri 7:13, "Tafakari vema kazi yake; kwa sababu ni nani awezaye kukinyoosha kitu kile alichokipotosha yeye?" -: Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira.
- Get link
- X
- Other Apps
TOPIC: “THE SPIRIT OF THE LORD UPON US.” The Spirit of the Lord upon us has carried two great things, which are; IDENTIFYING GOD TO PEOPLE and ANOINTING PEOPLE, where by God anoints us through Him. Jesus said that the Spirit of the Lord is upon Him, because He has anointed Him in order to preach the gospel or good news to the poor; so as to heal the brokenhearted, to preach deliverance to the captives and recovering of sight to the blind, to set at liberty them that are bruised, to preach the acceptable year of the Lord.” Luke 4:18 “The Spirit of the Lord is upon me, because he hath anointed me to preach the gospel to the poor; he hath sent me to heal the brokenhearted, to preach deliverance to the captives, and recovering of sight to the blind, to set at liberty them that are bruised, to preach the acceptable year of the Lord.” (KJV) The Spirit of the Lord was upon Him and pouring oil unto Him not inside Him; because He was sent by God who is our FATHER who is the Owner of the Heavens...
- Get link
- X
- Other Apps
SOMO: ROHO WA BWANA JUU YETU. Roho wa Bwana juu yetu, amebeba mambo Mawili makubwa, nayo ni KUMTAMBULISHA MUNGU KWA WATU na KUPAKA WATU MAFUTA; ambapo Mungu hutupaka Mafuta kupitia kwake. Yesu alisema Roho wa Bwana yu juu yake, ili kumtia Mafuta apate kuwahubiria maskini Injili au Habari njema. Apate kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao na vipofu kupata kuona tena. Awaache huru waliosetwa na kutangaza Mwaka wa Bwana uliokubaliwa. Luka 4:18-19 "Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia Mafuta kuwahubiria maskini habari njema, amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao......". Roho wa Bwana alikuwa juu yake akimmiminia mafuta, sio ndani yake; kwa sababu alitumwa na Mungu aliye BABA yetu, ambaye ndiye Mmiliki wa Mbingu na Nchi. Hiyo Mamlaka aliyonayo Mungu, amempa Bwana wetu Yesu Kristo ili apate kuwapa wale walio tayari kumtumikia Mungu, siku za uhai wao. Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.
- Get link
- X
- Other Apps
SOMO: ROHO WA BWANA JUU YETU. Roho wa BWANA juu yetu, ni moja ya Roho saba za Mungu zinazotenda kazi duniani, ambaye alihusika kuumba Mbingu na Nchi. Mwanzo 2:4 "Hivyo ndivyo vizazi vya Mbingu na Nchi zilipoumbwa. Siku zile BWANA Mungu alipoziumba Mbingu na Nchi". Vile vile ni kati ya Roho mbili zinazotolewa na Mungu mwenyewe, nyingine ni Roho wa Kumcha BWANA. Roho wa BWANA juu yako ni ili kukuwezesha kufanya Utumishi kwa Mungu wako aliyekurahisishia Maisha kwa kukupa Roho wake. Warumi 8:14 "Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu." Baada ya kufanyiwa hayo yote ndipo Mungu huruhusu Roho ya Kumcha BWANA, ili upate Kumcha YEYE, yaani upate kuwa na Ibada na Mungu wako. Mithali 8:17 "Nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona." Mathayo 5:8 "Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu." Kumpenda Mungu ndiyo moyo safi. Inaendelea..... Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira - Efa...
- Get link
- X
- Other Apps
"If you want to show the love of God to many by showing them how God loves His people; read the book of John and his Epistles, also read the book of Peter. You will see the Love of God and in return you will love people and the people will love you. The enmity between you and the people shall be destroyed." © Apostle & Prophet Josephat E. Mwingira (Efatha Ministry).
- Get link
- X
- Other Apps
Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira: Mungu anatafuta watu wanyenyekevu, walio tayari Kumwabudu ambao wanatetemeka wasikiapo habari zake. Kumcha BWANA ni kuchukia uovu na chochote kisichompendeza Mungu. Hali hii hukupa kuwa ushirika na Mungu, unaokufanya Kumpenda Mungu, Kumheshimu, Kumwabudu na Kumtumikia bila kulazimishwa. Unakuwa tayari kujitaabisha, kujituma na kujibidiisha kwa ajili ya BWANA, kwani ndiyo furaha yako. Unatimiza ahadi zako bila kuhimizwa, naye anatawala Maisha yako. Mtu wa Mungu anatakiwa awe na tabia hiyo, hahitaji abembelezwe ili amtumikie Mungu, awahi ibadani au amtolee Mungu. Unajua shida uliyonayo, kwa hiyo tenda kwa hiari ili ajibu haja ya moyo wako. Ukimpenda Mungu na kumtumikia kwa uaminifu na kweli; na kuwa na adabu mbele zake, utakuwa salama, mbali na uchungu, mahangaiko na kuonewa.