SOMO: KUBALI KUONGOZWA NA ROHO WA MUNGU.

Tukikubali kuongozwa na Roho wake tunafanyika kuwa Wana wa Mungu. Ukikubali kuongozwa na Roho wa Mungu, wana wa ibilisi watafanya kila wanaloweza ili kukuangamiza, kukufilisi,kukuaibisha, hata hivyo hawata fanikiwa, kwani Mungu atakufunika.

Ukikubali kuongozwa na Roho wa Mungu, unafanya kazi kama unavyotaka na unakuwa na NGUVU ya Kiungu ndani yako kwa kuwa Mwana wa Mfalme ni Mfalme na mtoto wa simba ni simba. Mhubiri 7:25-26 "Nikageuka, na moyo wangu ulikazwa katika kujua na kupeleleza, na kuitafuta hekima, na maana ya mambo yaliyoko; ili nifahamu ya kuwa uovu ni upumbavu, na upumbavu ni wazimu......".

Mwana hakamatwi na vitu vya kipumbavu, katika Mhubiri akasema, hii ni kama balaa katika nchi; wakuu wakitembea kwa miguu na watumwa wakipanda farasi! Hii ni balaa kubwa! Anamaanisha kuwa, wewe unayeitwa Mtoto wa Mungu umechoka huku wenye dhambi wakiendesha magari ya kifahari.

Mbingu na Nchi ni Mali ya BWANA ambaye ni BABA yako; Lakini umekuwa mchanga mpaka umeshindwa kumilikishwa. Pambana kutoka kwenye wokovu wa kirahisi rahisi; kubali kufundishwa ili ufike mahali pa kupambanua mwenyewe. Acha utoto maana watoto hawamiliki, bali wanatunziwa urithi. Jiulize wewe ni Mwana au ni Mtoto? Kubali kuongozwa na ROHO wa Bwana ili akufikishe mahali pa kumilikishwa yaliyo ya Baba yako wa Mbinguni.

Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira (EFATHA MINISTRY).

Comments