SOMO: NGUVU YA MUNGU.
NGUVU hii kazi yake ni kumiliki NGUVU zote zilizopo na inaweza kumfikisha mtu mahali pa kushangaza, kwa hiyo mtu asiseme hana NGUVU, tatizo ni kwamba hawezi kubaini NGUVU ipi inatumika wapi. Kuna NGUVU ya Mungu na ya uovu na huwezi kubaini NGUVU ya uovu kama hujaijua NGUVU ya Mungu.Ili uweze kujua uzuri wa NGUVU ya Mungu, ingia ndani maana ndani ya hiyo NGUVU, kuna Roho saba na kila Roho ina namna yake ya kutenda.
Ulipookoka ulipata NGUVU, lakini katika NGUVU hiyo, inahitaji IMANI. Ni kama ulipewa funguo unaofungua vyumba saba, yaani Roho saba za Mungu. Katika NGUVU hizi, unapewa kwanza ndogo ili uweze kufikia NGUVU kubwa. NGUVU ya Mungu inakuhamisha kutoka mahali pa uchache na kukuingiza mahali pa utele kwa hiyo huwezi kuwa maskini maana hairuhusu umaskini. NGUVU ya Mungu inaweza kusababisha utoke kwenye uchungu, ujinga, matatizo na mateso uliyonayo. Mtu hahitaji fedha, bali NGUVU ya Mungu, Maana hiyo ndiyo itakayo sababisha watu wamletee zawadi.
Comments
Post a Comment