MKESHA WA UDHIHIRISHO WA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU, EFATHA MINISTRY PRECIOUS CENTER KIBAHA,
Luka15:17 “Akawa akitamani kujishibisha kwa maganda waliyokula nguruwe, wala hapana mtu aliyempa kitu. Alipozingatia moyoni mwake, alisema, Ni watumishi wangapi wa baba yangu wanaokula chakula na kusaza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa.”
Mwana mpotevu alipata nafasi kwa Baba yake lakini akaichezea, ndiyo maana baada ya kuipoteza akajuta na kukumbuka nyumbani kwa baba yake, alijua kuwa nyumbani kwao kuna kila kitu ndiyo maana akaamua kurudi kwa Baba yake.
Vivyo hivyo ndivyo ilivyo Nyumbani mwa BABA yako wa Mbinguni, kuna chakula cha kutosha; rudi nyumbani kwa BABA yako ili uweze kupokea chakula kutoka kwake maana kwake kuna kila kitu unacho kitaka, ikiwemo Karama na Vipawa vya Roho Mtakatifu na chochote kile unacho kihitaji kinapatikana kwake.
© MCHUNGAJI BETSON KIKOTI.

Comments

Popular posts from this blog

Mithali 8:17-21 "Nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia. Matunda yangu hupita dhahabu, naam, dhahabu safi, na faida yangu hupita fedha iliyo teule. Natembea katika njia ya haki, katikati ya mapito ya hukumu. Niwarithishe mali wale wanipendao, tena nipate kuzijaza hazina zao." Proverbs 8: 17-21 "I love them that love me; and those that seek me early shall find me. Riches and honour are with me; yea, durable riches and righteousness. My fruit is better than gold, yea, than fine gold; and my revenue than choice silver. I lead in the way of righteousness, in the midst of the paths of judgment: That I may cause those that love me to inherit substance; and I will fill their treasures."