Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira:
Mungu anatafuta watu wanyenyekevu, walio tayari Kumwabudu ambao wanatetemeka wasikiapo habari zake. Kumcha BWANA ni kuchukia uovu na chochote kisichompendeza Mungu. Hali hii hukupa kuwa ushirika na Mungu, unaokufanya Kumpenda Mungu, Kumheshimu, Kumwabudu na Kumtumikia bila kulazimishwa. Unakuwa tayari kujitaabisha, kujituma na kujibidiisha kwa ajili ya BWANA, kwani ndiyo furaha yako. Unatimiza ahadi zako bila kuhimizwa, naye anatawala Maisha yako. Mtu wa Mungu anatakiwa awe na tabia hiyo, hahitaji abembelezwe ili amtumikie Mungu, awahi ibadani au amtolee Mungu. Unajua shida uliyonayo, kwa hiyo tenda kwa hiari ili ajibu haja ya moyo wako.
Ukimpenda Mungu na kumtumikia kwa uaminifu na kweli; na kuwa na adabu mbele zake, utakuwa salama, mbali na uchungu, mahangaiko na kuonewa.

Comments