Media
TRENET ni kituo cha television cha Kiroho kinachomilikiwa na Huduma ya EFATHA hapa Tanzania chini ya Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira.
Kituo hiki cha Television kilianzishwa mwaka 2007, kwa malengo ya kuhubiri Neno la Mungu, kueneza Habari Njema na kuelimisha jamii kupitia vipindi vyake. Baada kuanza kwa matangazo ya Digital, TRENET TV inaendelea kupatikana kupitia satelite BURE. Madishi kuanzia inch 6 yanaweza kupata Signals za TV yetu. Pia TRENET TV inapatikana katika King’amuzi cha TING HD Kinachomilikiwa na ATN hapa nchini.
TRENET TV inakusudia kueneza Neno la Mungu kwa kila kiumbe ili kila mtu asikie kwani ” Imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa Neno la Kristo” (Rumi 10:17)
Sikiliza IBADA, MAHUBIRI, MAFUNDISHO, NYIMBO na MATUKIO MBALIMBALI (Live) kutoka Efatha Ministry Mwenge, Dar es Salaam, Tanzania.
Comments
Post a Comment