MKESHA WA UDHIHIRISHO WA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU, EFATHA MINISTRY PRECIOUS CENTER KIBAHA:
Nguvu za ROHO MTAKATIFU zinapokuja kwetu, tunafaidiaka na nini.?
1. Katika UWEPO wake Roho Mtakatifu utajua mambo ya sasa na yale yajayo. Yohana 16:13 “Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.” Ukiijua KWELI ya Mungu ndiyo itakufanya uishi, Bwana Yesu akasema huyo Roho atakapokuja atawaingiza katika KWELI; kwa nini katika KWELI? Kwa sababu ndiyo itakayokupa KUISHI.
2. Utajua kuwa una BABA, MWANA na ROHO MTAKATIFU.
3. Utayajua yale mambo ambayo Umekirimiwa na BABA wa Mbinguni. 1 Wakorinto 2:12 “Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.” Mungu kila iitwapo leo ana jambo la kipekee kwa ajili yetu lakini sisi hatujui na ndiyo maana tunakufa maskini.
4. Roho huyu anapokuja kwako anakupa UJASIRI wa kulinena NENO la Mungu. Matendo 5:12 “Na kwa mikono ya Mitume zikafanyika ishara na maajabu mengi katika watu; nao wote walikuwako kwa nia moja katika ukumbi wa Sulemani;” Roho anapokuja NGUVU ya kuponya inadhihirika.
Inaendelea.........
© MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA.



Comments