SOMO: KUZINGATIA.
Luka 15: 11-32" Akasema, mtu mmoja alikuwa na wana wawili, yule mdogo akamwambia babaye, Baba, nipe sehemu ya mali inayo niangukia. Akawagawia vitu vyake.Hata baada ya siku si nyingi, yule mdogo akakusanya vyote, akasafiri kwenda nchi ya mbali, akatapanya mali zake huko kwa maisha ya uasherati........"
Mwana mpotevu alipozingatia moyoni mwake akafanya maamuzi ya kurudi kwa Baba yake, alisema ni kweli nimekosea lakini nitarudi. Na wewe leo usikubali kufa dhambini ondoka na urudi kwa Baba yako wa Mbinguni. Inawezekana unaishi na mume wa mtu, leo amua kuachana nae na urudi kama mwana mpotevu. Ondoa ile hali ya kusema nikiondoka watanionaje, au nitaishije? Yesu leo anakwambia rudi ATAKUPOKEA na yuko tayari KUKUSAIDIA.
Mwana mpotevu angeendelea kukaa kule angekufa huku anakula na nguruwe, lakini alipoamua kurudi Baba yake alimpokea akamvika vazi bora, njoo kwa Yesu akutue mizigo ya mateso na magonjwa, Mungu ameandaa USAIDIZI atakusaidia. Amua kumsikiliza Roho wa SHAURI maana anakupa kutengeneza, huyu ndiye Kiongozi wa Mabadiliko mruhusu atawale Maisha yako atakwambia hicho unachokifanya ni kibaya. Huu Mwaka usikupite bila kuona maajabu ya Mungu yakitokea kwako, na kinachozuia ni dhambi, dhambi inazuia usipokee uliyokusudiwa na Mungu.
Mtumishi wa Mungu Mama Eliakunda Mwingira - Efatha Ministry.

Comments