MKESHA WA UDHIHIRISHO WA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU, EFATHA MINISTRY PRECIOUS CENTER KIBAHA;
Huu ni mwaka wa nne wa Mtembeo wa Mungu, huu si Mtembeo wa Mwanadamu bali ni wa Mungu kutembea na watu wake wale ambao amewaridhia, hivyo basi huu ni mwaka wa udhihirisho wa Nguvu za Mungu; hutakaa utikiswe na chochote, shetani hatakaa akutishie tena kwa sababu una Nguvu za Mungu.
Matendo 1:8 “Lakini mtapokea NGUVU, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa MASHAHIDI wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.” Hii ni Ahadi ya Mungu kwa wale wanao mwamini Yesu Kristo, kama wewe ni mmoja wao Ahadi hii ni yako si ya shangazi yako wala mjomba wako.
Wewe unaye mwamini unapewa Ahadi hii ili uwe shahidi wa mambo ya Mungu kupitia Kristo Yesu; hivyo ukiipata NGUVU hiyo unakuwa na uwezo wa kujionyesha wewe ni muwakilishi wa Mungu huku duniani.
Wewe unaye mwamini unapewa Ahadi hii ili uwe shahidi wa mambo ya Mungu kupitia Kristo Yesu; hivyo ukiipata NGUVU hiyo unakuwa na uwezo wa kujionyesha wewe ni muwakilishi wa Mungu huku duniani.
Comments
Post a Comment