SOMO: USIDHARAU UUMBAJI WA MUNGU.
Kila alichoumba MUNGU kinakubalika mbele zake na kina Kusudi maalum kwa ajili yake, tena ni Watumishi wake. Ndani ya hicho kiumbe ameweka hazina ya VIPAWA.
Kwa hiyo usimdharau mtu kwa kuwa hujajua bado kesho atakuwa nani? au ana nini kitakachokusaidia au kukuokoa wakati wa uhitaji wako?
Tamani wengine wafikie Kusudi la Mungu katika Maisha yao kwa kuwasogeza karibu na Bwana. Chochote ambacho Mungu amekiweka mkononi au mbele yako, pokea na kitunze kwa shukurani kwa kuwa Kazi ya Mungu haina makosa.
Katika Biblia Nabii Balam aliokolewa na punda ambaye alimwona Malaika aliyetaka kumuua; Lakini yeye (Balam) hakumuona. 
Mungu anaweza kutumia kitu chochote ili kutimiza Mapenzi yake, maana anajua kila kinachotokea.
Mhubiri 7:13, "Tafakari vema kazi yake; kwa sababu ni nani awezaye kukinyoosha kitu kile alichokipotosha yeye?"
   -: Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira.

Comments