SOMO: NGUVU YA MUNGU.
Siri ya kupata NGUVU ya Mungu, ni kuishi maisha MATAKATIFU ili ukiomba Mungu apate kukusikia. Umaskini na ufukara ni dalili ya kuwa karibu na shetani kuliko Mungu. Kuipenda dunia na mambo yake, ni kumchukia Mungu na alama ya wazi ni hali ya umaskini. Amua kutafuta haki yake ili mengine uzidishiwe.
Hata hivyo hali halisi inaonyesha kuwa, watu wengi wako katika hali ya kukosa na kushindwa; tatizo ni kiwango kidogo cha ujuzi kuhusu makusudi na ahadi za Mungu juu yao na jinsi wanavyo kiri kinyume na mawazo ya Mungu. YEYE anatuwazia mambo mema; hivyo ni lazima kukiri vyema ili kufanya ulimwengu kutimiza kile tunachosema. Suluhisho ni kufanywa upya moyo na fikra, ili zimtii Mungu na Yesu Kristo kwa kuishi maisha MATAKATIFU.
   : Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira (Efatha Ministry.)



Comments

Popular posts from this blog

Mithali 8:17-21 "Nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia. Matunda yangu hupita dhahabu, naam, dhahabu safi, na faida yangu hupita fedha iliyo teule. Natembea katika njia ya haki, katikati ya mapito ya hukumu. Niwarithishe mali wale wanipendao, tena nipate kuzijaza hazina zao." Proverbs 8: 17-21 "I love them that love me; and those that seek me early shall find me. Riches and honour are with me; yea, durable riches and righteousness. My fruit is better than gold, yea, than fine gold; and my revenue than choice silver. I lead in the way of righteousness, in the midst of the paths of judgment: That I may cause those that love me to inherit substance; and I will fill their treasures."