SOMO: ROHO WA BWANA JUU YETU.

Roho wa BWANA juu yetu, ni moja ya Roho saba za Mungu zinazotenda kazi duniani, ambaye alihusika kuumba Mbingu na Nchi.
Mwanzo 2:4 "Hivyo ndivyo vizazi vya Mbingu na Nchi zilipoumbwa. Siku zile BWANA Mungu alipoziumba Mbingu na Nchi". Vile vile ni kati ya Roho mbili zinazotolewa na Mungu mwenyewe, nyingine ni Roho wa Kumcha BWANA. Roho wa BWANA juu yako ni ili kukuwezesha kufanya Utumishi kwa Mungu wako aliyekurahisishia Maisha kwa kukupa Roho wake.

Warumi 8:14 "Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu." Baada ya kufanyiwa hayo yote ndipo Mungu huruhusu Roho ya Kumcha BWANA, ili upate Kumcha YEYE, yaani upate kuwa na Ibada na Mungu wako.
Mithali 8:17 "Nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona." 

Mathayo 5:8 "Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu." Kumpenda Mungu ndiyo moyo safi.

Inaendelea.....

Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira - Efatha Ministry.

Comments