SOMO: TOFAUTI KATI YA MWANA NA MTOTO
Yohana1:12" Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio Jina lake". Ni vizuri ukafahamu tofauti ya MWANA na MTOTO na mazingira unayokwenda nayo. Tukimpokea Yesu Kristo; tunaitwa watoto wa Mungu na tukiendelea na WOKOVU, tunaitwa WANA wa Mungu. Watoto ni wale wasioelewa Neno la Mungu kwa kina. Biblia inasema wananyonya maziwa, hawajajua kupambanua Neno bado.
Ukiwa mtoto, unarushwa huku na kule, maana huna maamuzi, lakini unajengwa utoke kwenye utoto mpaka unafikia ukamilifu kwenye nafasi aliyoko Kristo. Wakamilifu ndio wanaoitwa WANA, ambao wanatenda kile angefanya Bwana Yesu, kama angekuwepo. Hawaitaji aje, bali wao wapo na wanamwakilisha Yesu hapa duniani. Kwa hiyo mtaani kwako ni lazima uonyeshe Bwana Yesu yupo.
Waliookoka ni jeshi la Bwana, na wale wachanga ni makuruta ambao hawajafika hatua ya kuwa maafande.Wakishamaliza hiyo hatua ya ukuruta na kufuzu, wanakuwa maafande, napo wanapanda daraja mpaka wanakuwa majenerali wakuu.Taka kupanda daraja na inategemea unavyokabili mambo au changamoto. Mtu akisha kuwa MWANA haangaiki kutafuta maombi maana Mungu ameshamtoa chini na kumpeleka juu.
   : Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira (EFATHA MINISTRY).

Comments