SOMO: KUZINGATIA.
Luka 15:14-18" Alipokuwa amekwisha tumia vyote, njaa kuu iliingia nchi ile, yeye naye akaanza kuhitaji. Akaenda akashikamana na mwenyeji mmoja wa nchi ile, naye alimpeleka shambani kwake kulisha nguruwe. Akawa akitamani kujishibisha kwa maganda waliyokula nguruwe, wala hapana mtu aliyempa kitu. ALIPOZINGATIA MOYONI MWAKE , akasema, Niwatumishi wangapi wa baba yangu wanaokula Chakula na kusaza....."
Mwana mpotevu alipozingatia moyoni mwake akafanya maamuzi yakurudi kwa baba yake. Kuna watu wanasema siwezi kuacha pombe, sigara, uzinzi au uasherati hii ni vita huwezi kuacha kirahisi lazima useme SITAKII. Kuna watu hawawezi kuishi maisha matakatifu kwa sababu ya vitu vya kupewa, wanapenda vitu vitamu, anasema nitaishije nikiacha dhambi?? Hebu amua kutoka hapo uone, MUNGU hatakuacha uaibike. Amua kufanya maamuzi ya hatari ili utoke kwenye hali inayokusumbua. Amua kurudi kwa BABA yako ambaye dunia na vyote viijazavyo ni mali yake, usiendelee kula na nguruwe wakati nyumbani kwa baba yako kuna utajiri wa kila aina.
Comments
Post a Comment