SOMO: KAZI ZA NGUVU YA MUNGU.

- Kukamilisha na Kufanikisha Maono ya Kiungu.
Yesu alipokuja duniani, alihitaji NGUVU ili kufanikisha Kazi yake. Ili tutoke kwenye misiba na shida tulizonazo, tunahitaji NGUVU ya Mungu. Musa alipowachukua wana wa Israel kutoka Misri kwenda Kaanan, alihitaji NGUVU ya Mungu ili kuwatoa.
Kutoka 7:8-13 "BWANA akanena na Musa na Haruni, akawaambia, jifanyieni miujiza; ndipo utakapomwambia Haruni, shika fimbo yako,........"

Bila NGUVU za Mungu, Musa asingeweza kuwashinda wale nyoka wa wachawi wa Farao na kuwatoa wana wa Israel Misri. Uzao wa Yakobo waliotoka Misri, ili wamiliki Kaanani, ilibidi watumie NGUVU ya Mungu kupigana na mataifa na ndivyo ilivyo hata sasa. Samsoni aliweza kuua dubu kwa taya la punda kwa NGUVU za Mungu. Waamuzi 14:5-6 "Ndipo Samsoni na baba yake na mama yake wakatelemkia Timna, wakafika mashamba ya mizabibu huko Timna; na tazama, mwana-simba akamngurumia. Roho ya BWANA ikamjilia kwa NGUVU, naye akampasua kana kwamba anampasua mwana-mbuzi, wala hakuwa na kitu chochote mkononi mwake; ....." Kwa NGUVU ya Mungu Daudi aliweza kuua simba, Dubu na Goliathi.

Tunahitaji NGUVU za Mungu ili kumshinda shetani na Nguvu zake tupate kutoka mahali pa makandamizo na kupata UHURU wa KWELI kwa kuingia kwenye UFALME wa Mungu.

: Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira - Efatha Ministry.

Comments