Posts

Showing posts from October, 2017
Image
SOMO: BADILISHA TABIA ZAKO: Wokovu ni kubadilika, inaumiza sana kuona mtu ameokoka na bado anaendelea na tabia za watu ambao hawajaokoka, hii inawafanya wale ambao hawajaokoka wakikuangalia wanasema kama kuokoka ndio hivyo basi. Imeandikwa kumpenda Mungu ni kuuchukia uovu. Wewe ambaye umeokoka umefanyika kuwa balozi wa Yesu hapa Duniani, watu hawamuoni Yesu bali wanakuona wewe, hivyo hakikisha tabia zako zinafanana na Yesu. Leo mwambie Yesu najichomeka kwako ili tabia zangu zifanane na Wewe, watu wakiniona waone wamekutana na Yesu. Mtumishi wa Mungu Mama Eliakunda Mwingira.
Image
SOMO: BADILISHA TABIA ZAKO: Ili uweze kuziona baraka za Mungu katika maisha yako, hakikisha tabia zako zinabadilika. Amua kuweka Neno la Mungu ndani yako, unapoliruhusu Neno la Mungu lifurike ndani yako linaondoa ile dhambi inayokutesa. Neno la Mungu ni kioo, ukiliangalia utajiona jinsi ulivyo na utabadilika. Haiwezekani Neno la Mungu likajaa ndani yako alafu ukawa mwizi, msengenyaji au mzinzi. Amua leo kuliruhusu Neno la Mungu lijae ndani yako kwa sababu Neno hilo ni maji litakusafisha na kukuondolea takataka zote. Mtumishi wa Mungu Mama Eliakunda Mwingira
Image
Naibariki Jumamosi yangu, SITAKUWA kama Nilivyokuwa tena, Mapato yangu YAMEBARIKIWA, Biashara zangu ZIMEBARIKIWA, Kazi zangu Ajira zangu ZIMEBARIKIWA, SITAKUWA kama Nilivyokuwa.
Image
SOMO: ROHO MTAKATIFU: Roho Mtakatifu anapokuja kwa mtu anamfanya huyo mtu kuwa MKAMILIFU. Ukamilifu ni nini? Ni kufanya vitu kwa usahihi bila kukosea, unapoanza biashara kama una Roho Mtakatifu hiyo biashara haitakufa bali huyu Roho ataikamilisha. Ukiwa na Roho Mtakatifu hata unapo oa au kuolewa, ndoa yako inakuwa na ukamilifu, haitakuwa na mitikisiko wala kuyumba bali inajaa ukamilifu na Upendo. Chochote kinacho milikiwa na Mungu kinaweza kuletwa kwako kupitia Roho Mtakatifu. Siku utakapojua namna ya kuwasiliana na Roho Mtakatifu mahangaiko yako yatakoma, kwani atakufunulia mambo yaliyofichika katika ulimwengu wa Roho. Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira.
Image
MTUMISHI WA MUNGU MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA : Kamwe usijinenee mabaya kwani itakuwa kama ulivyo jitamkia, unakuta mtu anakiri " siku hizi maisha ni magumu sana " unapo kiri hivyo kamwe maisha yako hayataweza kuwa Mazuri, kwa sababu umejitabiria maisha magumu mwenyewe. Usijitabirie mambo mabaya, mara nyingi akina Dada mnaweza kuwa na marafiki zenu mnaanza kusema, wanaume ni wabaya sana, alafu unataka kuolewa, hapo usitegemee kupata mume mzuri. Vijana wengine wanasema wanawake ni wasumbufu sana, ukisema hivyo usitarajie kupata mke mtulivu bali tarajia kupata kama yule uliyejitabiria mwenyewe. Unapaswa kuwa makini sana na maneno ya kinywa chako, chochote utakacho kiri kitakuwa kama ulivyo kiri.
Image
SOMO: NGUVU YA MUNGU : Yohana 14: 16" Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele. " Yohana 14: 26" Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa Jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia ". Huyu Roho Mtakatifu aliyebeba nguvu hii anawajibu mbili. 1. Anafundisha. Hakuna anayeishi kwa ajili ya jana bali tunaishi kwa ajili ya leo, hivyo tunamhitaji ili atufundishe namna tutakavyo kutana na kesho yetu, atufundishe kuhusu sasa na kesho. Hakuna atakaye kufundisha kuhusu jana maana jana imepita. Mafundisho ni kwa ajili ya leo na kesho. 2. Huyu Msaidizi atatukumbusha. Atakukumbusha kwa nini Wewe ni maskini, kwa nini hujaoa/kuolewa na kwa nini huzai. Roho atakukumbusha kilichowahi kutokea kinacho sababisha unateseka leo. Roho Mtakatifu ambaye amebeba Nguvu, anatufundisha kuhusu kesho maana kesho yetu ni njema sana, anatukumbusha ya jana ili yaliyotokea jana ...
Image
U MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA : SOMO: NGUVU YA MUNGU : Wewe ni wa muhimu sana kwa Mungu, maana alimtoa Mwanawe wa pekee ili aje hapa Duniani AKUFIE. Huu ni Mwaka wa kujibiwa Maombi kama alivyosema kwetu 2017 ni Mwaka wetu wakujibiwa Maombi. Matendo ya Mitume 1:8 "Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu.... " Yesu anasema mtapokea Nguvu akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu ili tuweze kuwa MASHAHIDI na ili tuweze kuzaa matunda. Hatuta weza kuzaa matunda kama hatufuati maagizo yake. Kwa nini ni muhimu kuwa na Nguvu ya Mungu? Kwa sababu Dunia imejaa giza, hivyo hutaweza kuwa na Nguvu na Utukufu kama huna Nguvu ya Mungu. Ulinzi wa Mungu unatokana na hii Nguvu vinginevyo wachawi watakuloga, watakufanya uwe supu yao, mapepo yatakukandamiza na roho ovu zitaishi ndani yako. Bila Nguvu ya Mungu huwezi kuudhihirisha Wokovu/Ukristo wako . Yesu anasema atatupa Nguvu ili tuwe na Ushuhuda
Image
Naibariki Alhamisi yangu, SITAKUWA kama Nilivyokuwa.
Image
Image
"Kabla HUJAOMBA au KUFUNGA, ni lazima kujua unamtumikia Mungu yupi, halafu TAFAKARI kwa nini Unafanya hivyo. Sisi Waamini wa YESU KRISTO tunamtumikia MUNGU MKUU." - Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.
Image
SOMO: NGUVU ZA MUNGU . Yeyote mwenye Neema na Nguvu za Mungu anaheshimiwa. Hata kama mume wako hajaokoka ukiwa na Neema na Nguvu za Mungu ukimwambia kitu atakusikiliza. Ukiwa na hiyo Nguvu adui zako watakimbia mbele yako, Mungu hatakuacha, wewe ni tishio katika mazingira yanayo kuzunguka. Unaenda kumiliki uridhi wako na kustawi sana. Omba Mungu akupe Nguvu zake maana ukiwa nazo unakuwa kichwa na sio mkia . Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira
Image
SOMO: NGUVU YA MUNGU . Nguvu ya Mungu ni tunda ambalo linapatikana baada ya Neema ya Mungu Kuja juu ya mtu. Katika uwepo wa mtembeo wa Nguvu ya Mungu, Roho ya uweza inakuwa kazini. Popote palipo na Nguvu ya Mungu Roho ya Uweza inakuwa Karibu. Nguvu ya Mungu inafukuza umaskini, inarahisisha kazi, inaondoa uchovu na kufanya mambo kuwa mepesi. Unapompokea Yesu kuwa Bwana na Mokozi wa maisha yako unaipata hiyo nguvu. Nguvu hii itakuinua juu na itakupa mahitaji yako na kukuondolea kila aina ya kudharauliwa. Ukiwa na Nguvu ya Mungu maisha yako yote hauta dharauliwa wala kupuuzwa. Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira.
Image
Naibariki Jumatano yangu, Mimi ni MSHINDI.
Image
MTUMISHI WA MUNGU MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA : Kutokana na ile taji ya miiba YESU aliyovalishwa kichwani mwake, mawazo yako yamekombolewa hivyo hutafikiria mambo madogo madogo, uovu hautakuwa kwako, huta jiona mdogo tena, wakati wote utajiona mtu mkuu na wakuu watasikiliza mausia yako. Mume/mke wako, familia yako na Boss wako watakusikiliza. Kuanzia sasa Wewe ni mshindi.
Image
SOMO : MATENDO YA NGUVU YA MUNGU: Kama NENO la MUNGU linakaa ndani yako chochote utakachosema kitakuwa kama ulivyosema. Kuanzia Leo naamuru NENO la MUNGU likae ndani yako ili utakapokuwa unaongea na Boss wako, jirani yako, mke /mume wako na adui yako akusikilize. Watu wenye Nguvu ya MUNGU wanapoongea katika mamlaka MUNGU anawasikikiliza kwa sababu mwenye mamlaka ni MUNGU. Kuanzia leo MUNGU atakusikiliza na lolote ulitendalo litafanikiwa. Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira.
Image
Watumishi wa Mungu wakiwa katika ibada ya Kuabudu katika Kusanyiko Kuu, Efatha Ministry Precious Center Kibaha.
Image
Mtumishi wa Mungu Mama Eliakunda Mwingira akimshukuru Mungu kwaajili ya Kusanyiko Kuu la tisa lililoanza tarehe 2/10/2017 mpaka leo tarehe 9/10/2017.
Image
Efatha Ministry Mass choir wakimwadhimisha Mungu katika Mkesha wa hitimisho la Kusanyiko Kuu la tisa unaoendelea hapa Efatha Ministry Precious Center Kibaha.
Image
KUSANYIKO KUU LA TISA EFATHA MINISTRY PRECIOUS CENTER KIBAHA SIKU YA MWISHO. Huwezi kusimama kinyume na ibilisi bila NGUVU ya Mungu. Unaweza kuona watu waliokoka kama ni watu waliopoteza muelekeo, ambao wamejaa na matatizo na mahangaiko ya kila aina, lakini hiyo si kweli, ukweli wa mambo ni kuwa watu waliiokoka ni washindi. Warumi 8:37 “Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. ” 1Yohana 5:4 “Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu. ” Wokovu ni Neema inayokupelekea wewe kuwa na Nguvu ya Mungu, hivyo unapo pata wokovu ambao tunapata kupitia Pendo la Mungu inakuwa ni rahisi kwako kufurahia Neema ya Mungu. Bwana Yesu alisema tangu siku za Yohana Mbatizaji mpaka siku ya unyakuo ni wale tu wenye Nguvu ya Mungu ndio watakaoweza kuuridhi Ufalme wa Mungu. Huwezi kuuridhi Ufalme wa Mungu au kula mema ya Mungu kama huna Nguvu zake. Huwe...
Image
Image
USHUHUDA: Naitwa Piensia Mapunda. Namshukuru sana Mungu kwa matendo yake makuu kwangu. Ndani ya miaka 15 niliishi mbali na mtoto wangu, na sikujua alipokuwa, kwa sababu hakukuwa na mawasiliano kati yangu na yeye. Siku moja akanipigia simu akaniambia kuwa anahali mbaya sana, lakini hakuniambia alikuwa wapi. Baadae nilikuja kufahamu kwamba alikuwa Tanga. Namshukuru Mungu, Baba yetu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira alisema mwaka huu ni mwaka wa kujibiwa maombi, nilipofika kule Tanga, nilimkuta amekuwa mvuta bangi na mlevi wala haeleweki. Nilifanikiwa kumleta Efatha na baada ya kumleta hapa amebadilika kwani amempokea Yesu.
Image
USHUHUDA: Naitwa Heshima John. Napenda kumshukuru Mungu kwa matendo yake ya ajabu kwangu. Ilikuwa mwaka 2016 nilivimba tumbo nikaenda kupima nikaambiwa nina ugonjwa wa Ini na HIV. Ndipo nikaja kwenye kusanyiko kuu la mwaka 2016,Baba Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akawaombea wagonjwa na mimi nikiwa mmoja wao. Baada ya kuombewa, nikakurudi katika eneo langu la kulala, nilishangaa nikaanza kulia mwenyewe, na baadae nikaanza kucheka pasipo kujua kilichokuwa kinanichekesha, kuanzia hapo tumbo langu likaanza kuuma na nilikojoa sana na kutapika. Tumbo likaisha lote na niliporudi nyumbani nikaenda kupima haukuonekana ugonjwa wowote ule. Napenda kumshukuru sana Mungu kwa matendo yake ya ajabu kwangu, Sifa na Utukufu anastahili yeye peke yake. Sina cha zaidi cha kumpa zaidi ya kumshukuru Mungu wangu.
Image
Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira na Mama Eliakunda Mwingira wakiwa katika ibada Efatha Ministry PRECIOUS CENTER KIBAHA:
Image
MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA. Nakutamkia hutakuwa kama ulivyo kuwa, kwa maana sisi tuliookoka shetani hana Nguvu kabisa juu ya maisha yetu, sasa je! ni yupi aliye adui mkubwa kwetu? Adui mkubwa wa maisha yako ni akili yako, fahamu zako na mwili wako mwenyewe, shetani ni aduni namba mbili. Chochote unacho kihitaji katika maisha yako kinawezekana Kama unataka kuwa mtu mkuu inawezekana, kama unataka kuwa mchawi pia inawezekana, maana Mungu ni mzuri sana amesema cho chote utakachoomba kwa Jina lake atakupa. Kama unataka kuwa chombo cha Mungu basi Mungu pia atakuletea watu wake kukusaidia ili uweze kufikia hapo . Kama unataka kuwa tajiri Mungu analeta Roho wake kukusaidia ili uweze kuwa tajiri. Kama unataka kuwa maskini Mungu atakusaidia ili uweze kuufurahia huo umaskini wako, na pia atakuletea wahubiri ambao watakusaidia kabisa kufikia lengo lako. Mungu anao uwezo wa kukupa chochote kile ambacho unakitaka je! wewe unataka nini? Ili uweze kupokea lazima...
Image
KATIKA PICHA : Ujio wa Mtumishi wa MUNGU Dr. Morris Cerullo, Efatha Ministry Precious Center Kibaha, ambapo amepokelewa na mwenyeji wake Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira na Mama Eliakunda Mwingira.
Image
KUSANYIKO KUU LA TISA, EFATHA MINISTRY PRECIOUS CENTER KIBAHA: ASKOFU: CHALRES KARIUKI - KUTOKA KENYA Kuna vitu ambacho walipaswa kumiliki Babu zako au wazazi wako lakini hawakumiliki kwa sababu walikuwa ng’ambo ya Yordani hivyo kwa kuwa wewe Mungu amekuvusha kila ambacho Mungu aliwapa babu zako au Baba yako na hawakumiliki ni cha kwako, wao hawakumiliki kwa sababu walikufa wakiwa upande wa pili wa Yordani. Mimi na wewe tunavuka ili kumiliki nchi yetu ya Ahadi. Baba zetu wali fia jangwani ili sisi tuweze kumiliki nchi ya Ahadi. Bwana Yesu aliuchukua umaskini wetu na kuupeleka msalabani na alipokuwa anasurubiwa alisema imekwisha. Pale msalabani umaskini wako ulishindwa, pale msalabani ulipata haki yako ya kumiliki , pale msalabani ulipokea afya njema na kila kitu unacho kihitaji katika maisha yako. Ibilisi ni muongo na hauelewi msalaba kwa sababu msalaba ni kwa ajili ya kuvuka, kuacha kila shida au matatizo na kuwa mzima na kumiliki. Biblia inasema alichukua udhai...
Image
KUSANYIKO KUU LA TISA, EFATHA MINISTRY PRECIOUS CENTER KIBAHA: ASKOFU: CHALRES KARIUKI - KUTOKA KENYA Marko 4:35 “Siku ile kulipokuwa jioni, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng'ambo. ” Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake na tuvuke ng’ambo. Kule Upande wa pili, Upande wa ng’ambo ni wa Ushindi, hakuna kushindwa bali ni upande wa kushinda. Mungu akamwambia Musa wewe uko ukingoni mwa Bahari, hawa watu wa Ibrahimu lazima waivuke hiyo Bahari ya Shamu mpaka ng’ambo ili waweze kurithi. Musa aliwaongoza wana wa Israel kuelekea nchi ya Ahadi. Wale ambao ulikuwa ni uzao mchanga walikuwa ni uzao wa Yoshua na Kalebu, lakini uzao uliotoka Misri ulikufa jangwani. Hivyo ilimbidi Musa na yeye afe ili ule uzao mchanga uweze kufika katika nchi ya Ahadi. Yoshua 12:7 “Hawa ni wafalme wa hiyo nchi ambao Yoshua na wana wa Israeli waliwapiga ng'ambo ya pili ya Yordani upande wa magharibi, .... ” Walipokuwa ng’ambo ya Yordani Musa aliwapiga wafalme wawili, Sihoni mfalme wa Waamori na ...
Image
APOSTLE & PROPHET JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA, SUBJECT: YOU WILL NEVER BE THE SAME AGAIN. The devil has no power at all to those who have received Jesus as there Christ and Savior. Who then is the greatest enemy of our lives? THE GREATEST ENEMY OF YOUR LIFE IS; your MIND and BODY. Satan is just the second enemy after your Mind and Body. Whatsoever that you need in your life is possible; whether you want to be great, rich, intelligent or poor, or a witch. Everything is possible with God; whatever you need he will bring assistance to help you have it. If you want to be the Lord’s vessel and servant, he will bring people to you who will teach you and help you to know how to serve God. If you want to be rich he will bring people towards you who will hold you and enable you to become rich. If you want to be poor, he will bring people to you who will give you stories about poverty and how sweet it is to be poor. God has the ability to give you whatever you want in l...
Image
KUSANYIKO KUU LA TISA, EFATHA MINISTRY PRECIOUS CENTER KIBAHA: ASKOFU: CHALRES KARIUKI - KUTOKA KENYA Baada ya Yesu kuhubiri kukawa usiku, akauacha mkutano na kuwaambia wanafunzi wake wavuke ng’ambo. Marko 4:35 “Siku ile kulipokuwa jioni, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng'ambo.” Kule ng’ambo kuna vitu vikubwa sana. Kuna mambo unapaswa kuyafahamu:- • Maarifa; nini maana ya maarifa? Ni kukusanya taarifa, yaani unakuwa na taarifa. Mtu anapokwenda shuleni kusoma inamaana kuwa anakusanya taarifa, lakini katika ile shule kuna kuhitimu na baada ya kuhitimu yule mwanafunzi anapewa nguvu ya kwenda kufanya yale ambayo amejifunza. Leo ni siku ya kuhitimisha, Mungu aliye Baba yetu atatupa Nguvu ya kwenda kutekeleza yale tulio jifunza. • Ufahamu; Ufahamu ni ile hali ya uelewa wa taarifa. Watu wengi wanakwenda shule na kupata Maarifa lakini hawapati Ufahamu. Ukapate ufahamu katika Jina la Yesu • Hekima; Hekima ni nini? Ni ile hali ya kukuwezesha kutenda kazi kwa vitendo...
Image
KATIKA PICHA: WATUMISHI WA MUNGU WAKIMUABUDU MUNGU KATIKA KUSANYIKO KUU LA TISA PRECIOUS CENTER KIBAHA.
Image
KATIKA PICHA: WAIMBAJI WA EFATHA MINISTRY MASS CHOIR WAKIMUADHIMISHA MUNGU KATIKA KUSANYIKO KUU LA TISA PRECIOUS CENTER KIBAHA.
Image
BISHOP CHALRES KARIUKI (8TH OCTOBER, 2017) 7TH DAY OF THE ANNUAL CONGREGATION AT PRECIOUS CENTRE KIBAHA. TOPIC: CROSS OVER TO THE OTHER SIDE. You know about this side of your life, but you need to cross over to the other side. The other side is a SIDE of VICTORY. (There is no failure in it). When Joshua crossed with the Israelites to the other side, the first gift that they got was Jericho. In the other side there are enemies sitting on your blessings, but fear not since the Lord will enable you to posses those blessings . - For you to be able to cross over to the other side, you need the Cross of Jesus. At the cross, your poverty and failures were overcome by Jesus. - At the cross Jesus cancelled our failures. On this side they don’t recognize you, but at the other side they will seek for you. Joshua 12:7-24"And these are the kings of the country which Joshua and the children of Israel smote on this side Jordan on the west, ......"; On this side the...
Image
BISHOP CHALRES KARIUKI (8TH OCTOBER, 2017) 7TH DAY OF THE ANNUAL CONGREGATION AT PRECIOUS CENTRE KIBAHA. TOPIC: CROSS OVER TO THE OTHER SIDE. Mark 4:35"And the same day, when the even was come, he saith unto them, Let us pass over unto the other side". During the day, the Lord spent much of his time teaching about the Kingdom, but in the evening after sending away the crowd, the Lord Jesus spoke to his disciples and went with them to the other side of the sea. Seven is a number of Perfection and a mark of a new beginning. On this seventh day of the Annual Congregation the Lord will cross with you to the other side. There are three important things; 1. KNOWLEDGE; its gathering of information. So you become informed. You spend so many years in school so as to gather information. But after the graduation day, they give you power to go and act upon what you have learnt the whole years. When you get knowledge you need understanding so as to understand that...
Image
USHUHUDA: Naitwa Grace Kauma kutoka Shalom, Napenda kumshukuru Mungu kwa kuniponya. Niliteseka kwa muda wa miaka miwili nikiwa naumwa tumbo sana. Nilipokwenda Hospitali nilifanyiwa Ultrasound na haikuoyesha kitu chochote. Madaktari wakaamua kunifanyia upasuaji. Baada ya ule upasuaji nikakaa miaka mitatu siwezi kufanya kitu chochote kile, ile hali ya kutokufanya kazi ilikuwa inanitesa sana. Nilipokuwa nikilala usiku nikawa nakula nyama, na nikiamka asubuhi siwezi kula kitu chochote zaidi ya kunywa pepsi mbili asubuhi, mchana na usiku, kwa siku nilikuwa na kunywa soda sita . Baada ya kuhangaika sana hadi kwa waganga ili nipone lakini sikupata uponyaji . Wakati nilipokuwa ninahangaika, Daktari alisema kuwa tatizo langu halieleweki na nisitegemee kuolewa, labda baada ya miaka 15 au 20, ndipo naweza kuolewa. Napenda kumshukuru Mungu nilipokuja Efatha, katika Kusanyiko la mwaka 2013 nilipokea uponyaji nikawa mzima. Katika Kusanyiko la mwaka 2014 nilikuwa Mbe...
Image
KATIKA PICHA: Mtumishi wa Mungu Mchungaji Ruffers Christiee Kutoka Efatha Ministry Pakistani pamoja na watumishi wengine wakiwa na Diary za Efatha Ministry za Mwaka 2017.
Image
USHUHUDA: Ester Musa, natokea Kimara. Kwa muda wa mwaka mmoja nilikuwa nahisi tumboni kuna kitu kinatembea na nilipokwenda Hospitali nikaambiwa kuwa mimi ni mjamzito japo nilikuwa naona siku zangu kama kawaida. Nilikuwa naingia kwenye siku zangu kwa siku tano lakini baada ya hali hii nikawa napata hedhi kwa siku mbili na damu ikawa ni kidogo sana. Nilipokuja katika Kusanyiko hili linaloendelea Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akasema kuwa "kuna mtu anahisi kama ana mtoto tumboni lakini huyo si mtoto bali ni pepo kuanzia saa hii uwe huru kwa Jina la Yesu". Mtu huyo alikuwa ni mimi nikapokea uponyaji saa ile ile. Napenda kumshukuru Mungu kwa kuniponya katika Kusanyiko hili, nimeuona mkono wake hata kabla kusanyiko halijaisha..
Image
9TH ANNUAL CONGREGATION EFATHA MINISTRY PRECIOUS CENTER KIBAHA .WORD BY: DR. MORRIS CERULLO Tanzania is for the Lord Jesus: My birth day was on 2nd October, 2017, now I am 86 years old. I have 71(seventy one) years in Ministry and 66 (sixty six) years old in Marriage. I was just a young boy without parents (orphan). I lost my mother while I was 2 (two) years old, my father was a drunk and he could not help me. The government of the state that I lived took the responsibility of taking care of my family and I was taken to an orphanage. When I was 15 years old, the God of Moses, Ibrahim, Jacob, Joshua and Elijah came to this young boy who was an orphan and took me to Jesus. At that age, the Lord was able to take me to Heaven, by my eyes I saw the same Glory of God that Moses saw. After that encounter with the Lord, I dedicated all my life to God. For these 70 (seventy) years, I have never QUITED or LOOKED BACK in SERVING GOD. One year ago, I was suffering...
Image
KUSANYIKO KUU LA TISA EFATHA MINISTRY PRECIOUS CENTER KIBAHA: NENO NA: DR. MORRIS CERULLO KUTOKA US: Tanzania ni Mali ya Bwana Yesu: Tarehe 2/10/2017 ilikuwa ni siku yangu ya kuzaliwa, nilikuwa natimiza miaka 86. Miaka 71 katika Huduma na miaka 66 ndani ya ndoa. Mimi nilikuwa ni kijana ambaye sina wazazi yaani (yatima). Nilimpoteza Mama yangu nikiwa na miaka miwili na Baba yangu alikuwa ni mlevi sana hivyo asingeweza kunisaidia. Serikali ya jimbo tulilokuwa tunaishi ikaichukua familia yangu na mimi nikalelewa katika kituo cha watoto yatima. Nilipotimiza umri wa miaka 15 nilimuomba Mungu, huyu Mungu wa Musa, Ibrahimu , Yakobo, Yoshua na Eliya akaja kwangu niliyekuwa yatima mdogo nikiwa na umri wa miaka 15 na akanileta kwa Yesu. Katika umri huo ndipo Mungu akanitoa katika kituo cha watoto yatima, akanichukua na kunipeleka Mbinguni na kwa macho yangu niliuona Utukufu ule ule wa Mungu ambao Musa aliuona. Baada ya yale maono nikatoa maisha yangu yote kwa Mungu...