USHUHUDA:
Naitwa Heshima John. Napenda kumshukuru Mungu kwa matendo yake ya ajabu kwangu. Ilikuwa mwaka 2016 nilivimba tumbo nikaenda kupima nikaambiwa nina ugonjwa wa Ini na HIV. Ndipo nikaja kwenye kusanyiko kuu la mwaka 2016,Baba Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akawaombea wagonjwa na mimi nikiwa mmoja wao.
Baada ya kuombewa, nikakurudi katika eneo langu la kulala, nilishangaa nikaanza kulia mwenyewe, na baadae nikaanza kucheka pasipo kujua kilichokuwa kinanichekesha, kuanzia hapo tumbo langu likaanza kuuma na nilikojoa sana na kutapika. Tumbo likaisha lote na niliporudi nyumbani nikaenda kupima haukuonekana ugonjwa wowote ule. Napenda kumshukuru sana Mungu kwa matendo yake ya ajabu kwangu, Sifa na Utukufu anastahili yeye peke yake. Sina cha zaidi cha kumpa zaidi ya kumshukuru Mungu wangu.

Comments

Popular posts from this blog

Mithali 8:17-21 "Nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia. Matunda yangu hupita dhahabu, naam, dhahabu safi, na faida yangu hupita fedha iliyo teule. Natembea katika njia ya haki, katikati ya mapito ya hukumu. Niwarithishe mali wale wanipendao, tena nipate kuzijaza hazina zao." Proverbs 8: 17-21 "I love them that love me; and those that seek me early shall find me. Riches and honour are with me; yea, durable riches and righteousness. My fruit is better than gold, yea, than fine gold; and my revenue than choice silver. I lead in the way of righteousness, in the midst of the paths of judgment: That I may cause those that love me to inherit substance; and I will fill their treasures."