SOMO: BADILISHA TABIA ZAKO:
Wokovu ni kubadilika, inaumiza sana kuona mtu ameokoka na bado anaendelea na tabia za watu ambao hawajaokoka, hii inawafanya wale ambao hawajaokoka wakikuangalia wanasema kama kuokoka ndio hivyo basi.
Imeandikwa kumpenda Mungu ni kuuchukia uovu. Wewe ambaye umeokoka umefanyika kuwa balozi wa Yesu hapa Duniani, watu hawamuoni Yesu bali wanakuona wewe, hivyo hakikisha tabia zako zinafanana na Yesu.
Leo mwambie Yesu najichomeka kwako ili tabia zangu zifanane na Wewe, watu wakiniona waone wamekutana na Yesu.
Mtumishi wa Mungu Mama Eliakunda Mwingira.

Comments

Popular posts from this blog

Mithali 8:17-21 "Nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia. Matunda yangu hupita dhahabu, naam, dhahabu safi, na faida yangu hupita fedha iliyo teule. Natembea katika njia ya haki, katikati ya mapito ya hukumu. Niwarithishe mali wale wanipendao, tena nipate kuzijaza hazina zao." Proverbs 8: 17-21 "I love them that love me; and those that seek me early shall find me. Riches and honour are with me; yea, durable riches and righteousness. My fruit is better than gold, yea, than fine gold; and my revenue than choice silver. I lead in the way of righteousness, in the midst of the paths of judgment: That I may cause those that love me to inherit substance; and I will fill their treasures."