SOMO: NGUVU YA MUNGU .
Nguvu ya Mungu ni tunda ambalo linapatikana baada ya Neema ya Mungu Kuja juu ya mtu.
Katika uwepo wa mtembeo wa Nguvu ya Mungu, Roho ya uweza inakuwa kazini. Popote palipo na Nguvu ya Mungu Roho ya Uweza inakuwa Karibu.
Nguvu ya Mungu inafukuza umaskini, inarahisisha kazi, inaondoa uchovu na kufanya mambo kuwa mepesi. Unapompokea Yesu kuwa Bwana na Mokozi wa maisha yako unaipata hiyo nguvu.
Nguvu hii itakuinua juu na itakupa mahitaji yako na kukuondolea kila aina ya kudharauliwa. Ukiwa na Nguvu ya Mungu maisha yako yote hauta dharauliwa wala kupuuzwa.
Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira.
Comments
Post a Comment