KUSANYIKO KUU LA TISA, EFATHA MINISTRY PRECIOUS CENTER KIBAHA:
ASKOFU: CHALRES KARIUKI - KUTOKA KENYA
Baada ya Yesu kuhubiri kukawa usiku, akauacha mkutano na kuwaambia wanafunzi wake wavuke ng’ambo. Marko 4:35 “Siku ile kulipokuwa jioni, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng'ambo.” Kule ng’ambo kuna vitu vikubwa sana.
Kuna mambo unapaswa kuyafahamu:-
• Maarifa; nini maana ya maarifa? Ni kukusanya taarifa, yaani unakuwa na taarifa. Mtu anapokwenda shuleni kusoma inamaana kuwa anakusanya taarifa, lakini katika ile shule kuna kuhitimu na baada ya kuhitimu yule mwanafunzi anapewa nguvu ya kwenda kufanya yale ambayo amejifunza. Leo ni siku ya kuhitimisha, Mungu aliye Baba yetu atatupa Nguvu ya kwenda kutekeleza yale tulio jifunza.
• Ufahamu; Ufahamu ni ile hali ya uelewa wa taarifa. Watu wengi wanakwenda shule na kupata Maarifa lakini hawapati Ufahamu. Ukapate ufahamu katika Jina la Yesu
• Hekima; Hekima ni nini? Ni ile hali ya kukuwezesha kutenda kazi kwa vitendo, Maarifa na Ufahamu. Unapo anza kutendea kazi kwa Maarifa na Ufahamu ndipo unapokea Hekima. Bwana akakupe uwezo wa kutekeleza Maarifa na Ufahamu ili uweze kupokea Hekima

Comments