SOMO: NGUVU YA MUNGU :
Yohana 14: 16" Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele. "
Yohana 14: 26" Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa Jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia ".
Huyu Roho Mtakatifu aliyebeba nguvu hii anawajibu mbili.
1. Anafundisha.
Hakuna anayeishi kwa ajili ya jana bali tunaishi kwa ajili ya leo, hivyo tunamhitaji ili atufundishe namna tutakavyo kutana na kesho yetu, atufundishe kuhusu sasa na kesho. Hakuna atakaye kufundisha kuhusu jana maana jana imepita. Mafundisho ni kwa ajili ya leo na kesho.
2. Huyu Msaidizi atatukumbusha.
Atakukumbusha kwa nini Wewe ni maskini, kwa nini hujaoa/kuolewa na kwa nini huzai. Roho atakukumbusha kilichowahi kutokea kinacho sababisha unateseka leo.
Roho Mtakatifu ambaye amebeba Nguvu, anatufundisha kuhusu kesho maana kesho yetu ni njema sana, anatukumbusha ya jana ili yaliyotokea jana yasitokee tena kwenye maisha yetu
Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

Comments