U MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA : SOMO: NGUVU YA MUNGU :
Wewe ni wa muhimu sana kwa Mungu, maana alimtoa Mwanawe wa pekee ili aje hapa Duniani AKUFIE.
Huu ni Mwaka wa kujibiwa Maombi kama alivyosema kwetu 2017 ni Mwaka wetu wakujibiwa Maombi.
Matendo ya Mitume 1:8 "Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu.... "
Yesu anasema mtapokea Nguvu akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu ili tuweze kuwa MASHAHIDI na ili tuweze kuzaa matunda. Hatuta weza kuzaa matunda kama hatufuati maagizo yake.
Kwa nini ni muhimu kuwa na Nguvu ya Mungu? Kwa sababu Dunia imejaa giza, hivyo hutaweza kuwa na Nguvu na Utukufu kama huna Nguvu ya Mungu.
Ulinzi wa Mungu unatokana na hii Nguvu vinginevyo wachawi watakuloga, watakufanya uwe supu yao, mapepo yatakukandamiza na roho ovu zitaishi ndani yako.
Bila Nguvu ya Mungu huwezi kuudhihirisha Wokovu/Ukristo wako . Yesu anasema atatupa Nguvu ili tuwe na Ushuhuda

Comments