USHUHUDA:
Naitwa Piensia Mapunda. Namshukuru sana Mungu kwa matendo yake makuu kwangu. Ndani ya miaka 15 niliishi mbali na mtoto wangu, na sikujua alipokuwa, kwa sababu hakukuwa na mawasiliano kati yangu na yeye.
Siku moja akanipigia simu akaniambia kuwa anahali mbaya sana, lakini hakuniambia alikuwa wapi. Baadae nilikuja kufahamu kwamba alikuwa Tanga. Namshukuru Mungu, Baba yetu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira alisema mwaka huu ni mwaka wa kujibiwa maombi, nilipofika kule Tanga, nilimkuta amekuwa mvuta bangi na mlevi wala haeleweki. Nilifanikiwa kumleta Efatha na baada ya kumleta hapa amebadilika kwani amempokea Yesu.

Comments

Popular posts from this blog

Mithali 8:17-21 "Nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia. Matunda yangu hupita dhahabu, naam, dhahabu safi, na faida yangu hupita fedha iliyo teule. Natembea katika njia ya haki, katikati ya mapito ya hukumu. Niwarithishe mali wale wanipendao, tena nipate kuzijaza hazina zao." Proverbs 8: 17-21 "I love them that love me; and those that seek me early shall find me. Riches and honour are with me; yea, durable riches and righteousness. My fruit is better than gold, yea, than fine gold; and my revenue than choice silver. I lead in the way of righteousness, in the midst of the paths of judgment: That I may cause those that love me to inherit substance; and I will fill their treasures."