USHUHUDA:
Ester Musa, natokea Kimara.
Kwa muda wa mwaka mmoja nilikuwa nahisi tumboni kuna kitu kinatembea na nilipokwenda Hospitali nikaambiwa kuwa mimi ni mjamzito japo nilikuwa naona siku zangu kama kawaida.
Nilikuwa naingia kwenye siku zangu kwa siku tano lakini baada ya hali hii nikawa napata hedhi kwa siku mbili na damu ikawa ni kidogo sana. Nilipokuja katika Kusanyiko hili linaloendelea Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akasema kuwa "kuna mtu anahisi kama ana mtoto tumboni lakini huyo si mtoto bali ni pepo kuanzia saa hii uwe huru kwa Jina la Yesu".
Mtu huyo alikuwa ni mimi nikapokea uponyaji saa ile ile. Napenda kumshukuru Mungu kwa kuniponya katika Kusanyiko hili, nimeuona mkono wake hata kabla kusanyiko halijaisha..

Comments