KUSANYIKO KUU LA TISA EFATHA MINISTRY
PRECIOUS CENTER KIBAHA SIKU YA MWISHO.
Huwezi kusimama kinyume na ibilisi bila NGUVU ya Mungu. Unaweza kuona watu waliokoka kama ni watu waliopoteza muelekeo, ambao wamejaa na matatizo na mahangaiko ya kila aina, lakini hiyo si kweli, ukweli wa mambo ni kuwa watu waliiokoka ni washindi. Warumi 8:37 “Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. ”
1Yohana 5:4 “Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu. ”
Wokovu ni Neema inayokupelekea wewe kuwa na Nguvu ya Mungu, hivyo unapo pata wokovu ambao tunapata kupitia Pendo la Mungu inakuwa ni rahisi kwako kufurahia Neema ya Mungu.
Bwana Yesu alisema tangu siku za Yohana Mbatizaji mpaka siku ya unyakuo ni wale tu wenye Nguvu ya Mungu ndio watakaoweza kuuridhi Ufalme wa Mungu.
Huwezi kuuridhi Ufalme wa Mungu au kula mema ya Mungu kama huna Nguvu zake. Huwezi kufurahia wema wa Mungu kama huna Nguvu zake, utaishia kuona watu wengine wakifanikiwa, wakiwa na magari na nyumba nzuri. Watu waliookoka si kwamba wanamtumikia Mungu ili waende Mbinguni tu bali wanafanya hivyo kwa sababu wanamfurahia Mungu wao, hivyo wanakuwa na Nguvu ya Mungu ya kuwawezesha kufanikiwa sana.
MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA

Comments