SOMO: BADILISHA TABIA ZAKO:
Ili uweze kuziona baraka za Mungu katika maisha yako, hakikisha tabia zako zinabadilika.
Amua kuweka Neno la Mungu ndani yako, unapoliruhusu Neno la Mungu lifurike ndani yako linaondoa ile dhambi inayokutesa. Neno la Mungu ni kioo, ukiliangalia utajiona jinsi ulivyo na utabadilika.
Haiwezekani Neno la Mungu likajaa ndani yako alafu ukawa mwizi, msengenyaji au mzinzi. Amua leo kuliruhusu Neno la Mungu lijae ndani yako kwa sababu Neno hilo ni maji litakusafisha na kukuondolea takataka zote.
Mtumishi wa Mungu Mama Eliakunda Mwingira

Comments