MTUMISHI WA MUNGU MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA :
Kamwe usijinenee mabaya kwani itakuwa kama ulivyo jitamkia, unakuta mtu anakiri " siku hizi maisha ni magumu sana " unapo kiri hivyo kamwe maisha yako hayataweza kuwa Mazuri, kwa sababu umejitabiria maisha magumu mwenyewe.
Usijitabirie mambo mabaya, mara nyingi akina Dada mnaweza kuwa na marafiki zenu mnaanza kusema, wanaume ni wabaya sana, alafu unataka kuolewa, hapo usitegemee kupata mume mzuri.
Vijana wengine wanasema wanawake ni wasumbufu sana, ukisema hivyo usitarajie kupata mke mtulivu bali tarajia kupata kama yule uliyejitabiria mwenyewe.
Unapaswa kuwa makini sana na maneno ya kinywa chako, chochote utakacho kiri kitakuwa kama ulivyo kiri.

Comments