USHUHUDA:
Naitwa Grace Kauma kutoka Shalom,
Napenda kumshukuru Mungu kwa kuniponya. Niliteseka kwa muda wa miaka miwili nikiwa naumwa tumbo sana. Nilipokwenda Hospitali nilifanyiwa Ultrasound na haikuoyesha kitu chochote. Madaktari wakaamua kunifanyia upasuaji. Baada ya ule upasuaji nikakaa miaka mitatu siwezi kufanya kitu chochote kile, ile hali ya kutokufanya kazi ilikuwa inanitesa sana.
Nilipokuwa nikilala usiku nikawa nakula nyama, na nikiamka asubuhi siwezi kula kitu chochote zaidi ya kunywa pepsi mbili asubuhi, mchana na usiku, kwa siku nilikuwa na kunywa soda sita . Baada ya kuhangaika sana hadi kwa waganga ili nipone lakini sikupata uponyaji .
Wakati nilipokuwa ninahangaika, Daktari alisema kuwa tatizo langu halieleweki na nisitegemee kuolewa, labda baada ya miaka 15 au 20, ndipo naweza kuolewa. Napenda kumshukuru Mungu nilipokuja Efatha, katika Kusanyiko la mwaka 2013 nilipokea uponyaji nikawa mzima.
Katika Kusanyiko la mwaka 2014 nilikuwa Mbeya Baba Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akatangaza “ watu wengi wanaenda kuoa na kuolewa” na mimi nilikuwa namsikiliza nikiwa Mkoani Mbeya, nikasema na mimi ni mmoja wao.
Tarehe 10/7/2015 nilifunga ndoa katika Madhabahu ya Efatha, namshukuru sana Mungu kwani ameondoa aibu yangu na ibilisi ameshindwa. Nawashauri ndugu zangu msisisikilize kile ambacho watu au Madaktari wana waambia kuwa haiwezekani, bali mwangalieni Mungu kwani anaweza yote.

Comments