Posts

Showing posts from September, 2017
Image
Haleluya, Naibariki Alhamisi yangu, YESU KRISTO Aliye BWANA na MWOKOZI Wangu ni MZURI, MUNGU BABA YANGU wa MBINGUNI ni MZURI, ROHO MTAKATIFU Mwalimu wangu na Kiongozi wangu ni MZURI, Haleluya, Mimi ni MFALME, Mimi ni KUHANI wa BWANA, Nitatembea KIFALME, Nitamiliki KIFALME, Nitaishi MAISHA MATAKATIFU ili NIMFURAHISHE na KUMPENDEZA MUNGU Aliye BABA Yangu PEKEE wa MBINGUNI, Kicheko, Furaha, Amani, Afya Njema tena ya KUDUMU, Upendo, KUTOKUSHINDWA Vitanizungukaaaaa Maana BABA YU PAMOJA NAMI, Na ANANIPENDA, Furahi Mwanangu ALHAMISI yako IMEBARIKIWA.
Image
KUSANYIKO KUSANYIKO KUSANYIKO LA BWANA 2017. Kwa Wageni wote na wale wenye Mapenzi mema, ndani na nje ya Nchi ambao watapenda kuhudhuria hili KUSANYIKO KUU 2017, mnaweza Kujiandikisha ONLINE kupitia Website ya Huduma (  www.efathaministry.org  ) na kufuata Maelekezo yote ambayo yametolewa.
Image
ARE YOU READY TO CHANGE THE DIRECTION OF WHAT YOU HAVE HEARD (Second part). REFUSE and DELETE from your MIND and MEMORY any information which you have ever heard or which you will hear or which you are Hearing that shows FAILURE or DESTRUCTION; what do I mean by that? REFUSE to listen to someone who says...... “mmmmh; You know I was once married, eeeh..... that man is very awkward, we ended up divorcing....! If you sit with such a person, you will also FAIL in your marriage , and if you are not married, you will NEVER marry. If you see her starting to tell you, .... “my friend, don't be amazed; I was at once married" You were married? Eeeenh..... “But we divorced''...... you divorced eeenh? God Bless you, GOOD BYE,.... Depart from him or her and NEVER listen to such a person, because his or her words will DESTROY you or will create DESTRUCTION in you. If you see your fellow girl or boy, and you see her being pregnant or has impregnated a girl. Once you ask him/...
Image
UKO TAYARI KUBADILISHA MUELEKEO WA KILE ULICHOKISIKIA: (Sehemu ya Nne). Tumia MUDA wako mwingi katika kile ambacho unataka KIKUPE FAIDA, chukua Kalamu na Daftari, Haleluya, Chukua Kalamu na Daftari uwe una CHORA kila saa Muundo wa Serikali yako ya Kampuni, Muundo wa Utendaji, Namna utakavyoendesha Biashara zako, Unaandika kwenye Daftari lako, unalifunga, unaliweka Pembeni, Unakaa baada ya Miezi miwili tena, unachukua Daftari lingine, UNAPANGA tena, Unakumbuka Vizuri au Utakuwa umesahau, Unarudia tena, Unaweka pembeni, unakaa tena Mwezi mwingine, UNAUMBA tena, mpaka Unaona KWELI SASA kila kitu KIMEKAA. :- Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Mwenge Dar es Salaam, Tanzania, EFATHA MINISTRY.
Image
ARE YOU READY TO CHANGE THE DIRECTION OF WHAT YOU HAVE HEARD? Decide to change THE PERCEPTION of your HEARING, by listening only to the things which will help BUILD the best of your Future. Change the perception of your hearing. Desire to HEAR that which will only cause the BEST out of your life in the FUTURE. Desire to LISTEN, CO-OPERATE and DO things with the people who have SUCCEEDED, WON and FLOURISHED in the same environment which you are in. :- The Servant of GOD Apost le and Prophet Josephat Elias Mwingira, Mwenge Dar es Salaam, Tanzania, EFATHA MINISTRY. (Will continue............)
Image
UKO TAYARI KUBADILISHA MUELEKEO WA KILE ULICHOKISIKIA: (Sehemu ya Tatu). Tengeneza GOAL yako, Tengeneza GOAL, AMEN? Unataka kuwa NANI WEWE? Unataka KUFIKA WAPI WEWE? Tengeneza GOAL for your Achievement, sawa? Tengeneza GOAL yako. Kwa kufanyaje? Kwa KUBUNI namna gani unataka UFIKE mahali Fulani, na weka Mkazo na Msisitizo katika hicho UNACHOAMINI unataka KITOKEE. :- Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Mwenge Dar es Salaam, Tanzania, EFATHA MINISTRY.
Image
UKO TAYARI KUBADILISHA MUELEKEO WA KILE ULICHOKISIKIA: (Sehemu ya Pili). KATAKAA na UZIFUTE kwenye AKLI YAKO na UFAHAMU WAKO Habari zote ulizowahi Kuzisikia au Utakazozisikia au Unazozisikia zinazoonyesha KUSHINDWA au UHARIBIFU; nina maanisha Nini hapo? USIKUBALI KUMSIKILIZA Mtu anayesema …. “mmmh Unajua Mimi niliolewaga, eeeh…. Mmh yule Mwanaume balaaa, Nikaondoka mwenyewe….” Ukikaa naye huyo Mtu, na WEWE UTAONDOKA katika Ndoa yako, UKIMSIKILIZA huyo Mtu….. Na WEWE UTAONDOKA  katika NDOA yako, na Kama hujaolewa…Hutakaa UOLEWE. We Ukimuona tu anaanza KUKUAMBIA, … “Mwenzangu usinione hivi Niliolewaga miye” … Uliolewa? Eeeenh… “Mmmh Sasa hivi tuliachanaga” ….. Mliachana eeenhh? MUNGU Akubariki KWAHERI, …. MUAGE Mapema UENDE Zako USIMSIKILIZE, maana lazima Ataumba UHARIBIFU kwako. Ukiona Binti mwenzio au Mkaka mwenzio, unamuuliza vipi Mbona Mjamzito Ndoa mmefunga lini?,…. Anakuambia “ aaah Ndio hivyo ilitokea tu, nilikuwa….” MKIMBIE, USISIKILIZE, UKIMSIKILIZA huyo Mtu na Wewe ...
Image
THE LORD’S PRAYER. Philipians 4:8 " Finally, brethren, whatsoever things are true, whatsoever things are honest, whatsoever things are just, whatsoever things are pure, whatsoever things are lovely, whatsoever things are of good report; if there be any virtue, and if there be any praise, think on these things.Those things, which ye have both learned, and received, and heard, and seen in me, do: and the God of peace shall be with you". • Whatsoever that is honest; make sure t hat you do things that are honest for others, don’t do things that will make you alone to be happy; make sure that you do things that will make other people to praise your God, don’t be selfish but do things that will benefit others.  • Whatsoever that is just; Make sure that you are just. You are the Lord’s RIGHTEOUS one, so make sure that others see that you are carrying his RIGHTEOUSNESS. Don’t speak stupid things which will make people question you; but do things that will make others to REPENT b...
Image
SOMO: SALA YA BWANA. Wafilipi 4:8 ” Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo. • YO YOTE YALIYO YA STAHA: Hakikisha unafanya mambo ya STAHA kwa ajili ya wengine, usifanye mambo kwa kujifurahisha wewe mwenyewe hakikisha unawapendeza wengine ili wamsifu Mungu wako, usiwe mbinafsi bali fanya mambo kwa ajili ya wengine. • YO YOTE YALIYO YA HAKI: Hakikisha unakuwa mwaminifu, wewe ni HAKI ya Mungu hivyo onyesha kuwa umeibeba ile HAKI ya Mungu, usiseme mambo ya kipumbavu au ambayo watu watakulaumu, fanya mambo ambayo yatafanya watu WAFIKIE TOBA sababu wewe ni MWENYE HAKI wa Mungu. Usifanye jambo kwa kuogopa watu, fanya jambo kwa kumuogopa Mungu wako tu, acha wakuone kuwa wewe unamuogopa Mungu. Upo hapo ulipo, katika sehemu ya chini kabisa kwa sababu humuogopi Mungu bali unawahofu watu, siku u...
Image
THE LORD’S PRAYER. What is God’s will? The WILL of God is that, you do GOOD things. Philipians 4:8-9 "Finally, brethren, whatsoever things are true, whatsoever things are honest, whatsoever things are just, whatsoever things are pure, whatsoever things are lovely, whatsoever things are of good report; if there be any virtue, and if there be any praise, think on these things. Those things, which ye have both learned, and received, and heard, and seen in me, do: and the God of  peace shall be with you". The things you do will cause God to come and dwell in you or to depart from you. Ask yourself; what do you want? Do you want God to DWELL in you or do you want God to DEPART from you. • If there’s no TRUTH in a thing, stay away from it. If you are surrounded by people who don’t carry the TRUTH in them, stay away from them; if you want God to DWELL with you. When Daniel and his fellows were given the King’s food which was good, they knew that in that food there was no TRU...
Image
THE LORD’S PRAYER. Mathew 6:9"After this manner therefore pray ye: Our Father which art in heaven, Hallowed be thy name" . The bible tells us to pray to our father in heaven not to the angels or to the saints on earth or in heaven. The Lord Jesus taught us that we are his, and that the Father in heaven chose us so that we may be his. The father in heaven has chose us so that we may be his sons and daughters; so we don’t have to pray through somebody else or to use another per son so as to reach our father in heaven, but we have to go straight by ourselves to the Father in heaven since he is our Father and we have been granted to ask him anything; so that Lord Jesus has told us that we should pray through his name and we shall receive whatever we ask. THY KINGDOM COME; The Kingdom of God comes when the Lord’s WILL comes in you, and when you act accordingly, is when the Kingdom of God comes in you. There are things that you have to do so as to allow the Kingdom of God to ...
Image
SOMO: SALA YA BWANA. MAPENZI ya Mungu ni nini? Mapenzi yake ni wewe utende Mema. Wafilipi 4:8-9” Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo.” Yale mambo Unayofanya yataweza kumsababisha Mungu aje akae ndani yako au kumuweka mbali na wewe. Wewe unataka nini? Mungu afanye makao kw ako au aondoke ? Nia yako wewe ni nini? Kama hamna KWELI katika kitu au jambo ufanyalo hilo jambo achana nalo. Kama upo na watu ambao hawana KWELI ndani yao achana nao, kama unataka Mungu awe na wewe. Danieli na wenzake walipopewa chakula kizuri cha Mfalme walijua kuwa katika chakula hicho hakukuwa na KWELI ndani yake, hivyo wakaamua kuachana nacho na wakakataa kula na wakala chakula cha kienyeji kabisa na wakawa na Nguvu na akili kuliko wenzao. Chochote ambacho unaona kuwa HAKINA KWELI ndani yake usikifanye ...
Image
Watumishi wa Mungu Ibadani Jumapili Efatha Ministry Mwenge, Dar es Salaam, Tanzania.
Image
SOMO: SALA YA BWANA. Mathayo 6:9 “Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, ” “Kwa kuwa Ufalme ni wako na Nguvu na Utukufu hata milele Amen.” Biblia inasema ombeni kwa Baba yenu wa Mbinguni si kwa Malaika, Watakatifu waliopo Duniani au Mbinguni, Hapana. Bwana YESU alitufundisha sisi kwa sababu ni wake na YEYE alituchagua ili tuwe wake na tumekubaliwa, hivyo Baba wa Minguni ametukubali ili tuwe Wana kwake. Hatuhitaji kuomba kupitia kwa (niaba) mtu fulani bali tunapaswa kwenda moja kwa moja kwa Mungu kwani tumeruhusiwa, na Bwana YESU ametuambia tuombe kwa JINA lake nasi tutapewa. UFALME wako uje; Ufalme wa Mungu unakuja pale Mapenzi ya Mungu yanapokuja ndani yako, na unapotenda sawasawa ndipo UFALME utakapokujilia ndani yako. Kuna mambo unahitaji kufanya ili usababishe au uruhusu UFALME ukujilie, ule UTUKUFU wa Mungu Mkuu huwa unakuja pale Nguvu na Utukufu zinapojidhihirisha kwako. Mathayo 7:18 “Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabay...
Image
UKO TAYARI KUBADILISHA MUELEKEO WA KILE ULICHOKISIKIA ?: "Amua kubadilisha MTAZAMO wako wa KUSIKIA, Amua KUBADILISHA Mtazamo wako wa KUSIKIA, kwa Kusikia yale tu ambayo YATAJENGA Ubora wa Ubadae wako, badilisha Mtazamo wako wa Kusikia. Tamani KUSIKIA yale tu ambayo yatasababisha UBORA wa Maisha yako ya Baadae. Tamani KUWASIKILIZA, KUSHIRIKIANA nao, KUFANYA nao Wale Watu ambao WAMEFANIKIWA, WAMESHINDA, WAMESITAWI katika Mazingira yale yale ambayo Wewe upo." (Itaendelea.......) :- Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.
Image
Hallelujah, Hallelujah, Hallelujah the Holy Annual Gathering 2017 is near,........for all our Guest World wide can register to attend this HOLY ANNUAL GATHERING through our Official Website  www.efathamistry.org  for Accommodation arrangement. Welcome ALL, our Mighty Heavenly Lovely FATHER Loves You.
Image
HALELUYA, HALELUYA, HALELUYA Kusanyiko TAKATIFU la Mwaka huu 2017 wa Kujibiwa MAOMBI Linakaribia. Kusanyiko litaanza tarehe 2/October - 8/ October, Kibaha Precious Centre Mji wa BWANA. Kwa Wale ambao ni Wageni (Si Wana Efatha Ndani ya Tanzania na Nje ya Tanzania) na wengependa kuja KUPOKEA kile ambacho BABA YETU KIPENZI WA MBINGUNI Alichoandaa kupitia Wapakwa Mafuta wake wakiongozwa na Mtumishi wake Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, unapaswa KUJIANDIKISHA (REGISTER YOUR  DETAILS) kupitia Website ya Huduma ambayo ni  www.efathaministry.org  kwa ajili ya Maandalizi ya Nafasi yako ya HOTEL (Malazi na Chakula) na kama pia utakuja na kuondoka (yaani hutalala) pia unapaswa KUJIANDIKISHA kwa ajili ya Utaratibu wa USAFIRI. Mwisho wa Kujiandikisha ni tarehe 22/ September Mwezi huu. Ukisha JIANDIKISHA utapokea E-mail yenye maelezo yote, pia unaweza kupata Maelezo yote katika Website yetu ya Huduma. UBARIKIWE Mwana wa Mungu, YESU Anakupenda, YESU Anakujali. "SHARE ...
Image
SOMO: NGUVU YA MEMA NA MABAYA. Ziko NGUVU mbili ambazo zinafanya Kazi katika ulimwengu wa Roho, hizi NGUVU mbili zinavutana kila iitwapo leo Nazo ni.  - Nguvu ya MEMA na   - Nguvu ya MABAYA Nguvu hizi haziwezi kuonekana kwa macho lakini tunaziona kupitia MATENDO ya mtu. Kuna MATENDO yakifanyika unapata kujua haya ni ya Roho MBAYA au Roho NZURI, yale ya Roho nzuri ni yale yaliyotendwa katika ROHO MTAKATIFU, yale ya roho mbaya yametendwa katika yule roho mchafu. Tunaweza ku baini NGUVU ya MEMA na MABAYA kupitia matendo ya mtu kwa sababu hatuwezi kuziona hizi roho mbili kwa macho ya kawaida. Kuna mtu akiona watu wanagombana anasikia kuumia, lakini kuna mwingine anafurahi watu wanapogombana, hivyo unajua tu ni Roho gani anayetenda kazi ndani yake. Mungu ni Roho na ni Mtakatifu sana hivyo amua kuwa Mtakatifu kama YEYE ili uweze kutenda Matendo MEMA maana pasipo huo Utakatifu hatutaweza kumpendeza MUNGU. :- Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira -EFA...
Image
SOMO : NGUVU YA MEMA NA MABAYA. MUNGU ni ROHO haonekani kwa macho haya ya damu na nyama, ni NEEMA Kama ukijaliwa kuona mambo ya MUNGU au WEMA wa MUNGU hata ukafikia hatua ya KUAMINI. Tunamjuaje MUNGU? Tunamjua MUNGU kupitia MATENDO yake, Matendo ndiyo yanayotupa kutambua aliyefanya jambo ni MUNGU au LA!. Kuna mambo yakifanyika kila mmoja anasema, "Huyu aliyefanya haya ni MUNGU ". Pia kuna mambo ambayo yakifanyika unajua aliyefanya si MUNGU. Ni kwa NEEMA tu ndipo tunaweza Kumjua MUNGU na Kumwamini, pasipo NEEMA ni ngumu kupambanua mambo ya MUNGU. :- Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira - EFATHA MINISTRY.
Image
ZIARA YA KITUME NA KINABII - ZANZIBAR (IKULU). PICHANI: Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira na Makamu wa Raisi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Balozi Seif Ali Iddi Ikulu, Zanzibar.
Image
ZIARA YA KITUME NA KINABII - ZANZIBAR (IKULU). PICHANI: Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira na Makamu wa Raisi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Balozi Seif Ali Iddi Ikulu, Zanzibar.
Image
ZIARA YA KITUME NA KINABII - ZANZIBAR (IKULU). PICHANI: Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Mwalimu Mama Eliakunda Mwingira, Makamu wa Raisi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Balozi Seif Ali Iddi, Waziri wa Nchi Mh. Mohamed Aboud Mohamed, Mchungaji Kiongozi wa Zanzibar Mch. Herry Nelson, pamoja na Watumishi wa Mungu Wachungaji Viongozi na Watendaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakipiga Picha ya pamoja, Ikulu Zanzibar.
Image
ZIARA YA KITUME NA KINABII - ZANZIBAR (IKULU). PICHANI: Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akifanya Maombi (AKIOMBA) Ikulu, Zanzibar.
Image
ZIARA YA KITUME NA KINABII - ZANZIBAR (IKULU). PICHANI: Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akiwa Ikulu na Makamu wa Raisi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Waziri wa Nchi Mh. Mohamed Aboud Mohamed na Viongozi wengine Watendaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Image
ZIARA YA KITUME NA KINABII - ZANZIBAR (IKULU). PICHANI: Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akiwa Ikulu na Makamu wa Raisi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Waziri wa Nchi Mh. Mohamed Aboud Mohamed na Viongozi wengine Watendaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Image
ZIARA YA KITUME NA KINABII - ZANZIBAR (IKULU). PICHANI: Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira na Makamu wa Raisi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Waziri wa Nchi Mh. Mohamed Aboud Mohamed na Viongozi wengine Watendaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Ikulu Zanzibar.
Image
ZIARA YA KITUME NA KINABII - ZANZIBAR (IKULU). PICHANI: Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akimkabidhi Kitabu cha "MOYO WA KIONGOZI" Makamu wa Raisi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Balozi Seif Ali Iddi.
Image
ZIARA YA KITUME NA KINABII - ZANZIBAR (IKULU). PICHANI: Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akisaini Kitabu chake cha "MOYO WA KIONGOZI" kwa ajili ya Kumpatia Zawadi Makamu wa Raisi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Balozi Seif Ali Iddi, Ikulu Zanzibar.
Image
ZIARA YA KITUME NA KINABII - ZANZIBAR (IKULU). PICHANI: Vyombo mbalimbali vya Habari vya nchini Zanzibar vikichukua Habari katika Mkutano/ Mazungumzo na Makamu wa Raisi wa Zanzibar Mh. Balozi Seif Ali Iddi na Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Ikulu Zanzibar.
Image
ZIARA YA KITUME NA KINABII - ZANZIBAR (IKULU). PICHANI: Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akiwa Ikulu na Makamu wa Raisi wa Zanzibar Mh. Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Waziri wa Nchi Mh. Mohamed Aboud Mohamed na Viongozi wengine Watendaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Image
ZIARA YA KITUME NA KINABII - ZANZIBAR (IKULU). PICHANI: Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akiwa Ikulu na Makamu wa Raisi wa Zanzibar Mh. Balozi Seif Ali Iddi  na Waziri wa Nchi Mh. Mohamed Aboud Mohamed na Viongozi wengine Watendaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Image
Naibariki Ijumaa yangu, Ijumaa yangu IMEBARIKIWA, Kazi zangu ZIMEBARIKIWA, Heshima yangu IMEBARIKIWA, Ndoa yangu IMEBARIKIWA, Nitaishi KIFALME, Nitatembea KIFALME, Nitaishi Maisha MATAKATIFU ili Nipate KUMFURAHISHA na KUMPENDEZA MUNGU BABA yangu wa Mbinguni, YEYE ni MWANZO na MWISHO, Hakuna kama YEYE......Haleluya, Nakupenda BABA, WEWE NI MZURI MUNGU WANGU, Nakupenda, Ijumaa yangu IMEBARIKIWA.
Image
Naibariki Jumamosi yangu, Jumamosi yangu IMEBARIKIWA, Mimi NIMEBARIKIWA, na Mapato yangu YAMEBARIKIWA, Biashara zangu ZIMEBARIKIWA, Kazi zangu ZIMEBARIKIWA, Wateja wangu WAMEBARIKIWA, Vyanzo vyangu Vyoote vya Mapato VIMEBARIKIWA, YESU WEWE Ni Mzuri, MUNGU BABA WEWE Ni Mzuri, ROHO MTAKATIFU WEWE Ni Mzuri, NAWAPENDA, Nakushukuru MUNGU BABA, Nakupenda, AMEN.
ZIARA YA KITUME NA KINABII EFATHA MINISTRY – ZANZIBAR; Ili uweze kuwa mshindi wa kesho yako ni lazima ujue Biblia inasemaje kuhusu hiyo kesho yako, Mwanzo 1:14 “Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya MCHANA na USIKU; nayo iwe ndiyo dalili na MAJIRA na SIKU na MIAKA;” Biblia inasemaje kuhusu usiku na mchana? Kuna mianga iliyotenga kati ya Usiku na Mchana, Usipo kuwa na UFAHAMU utashindwa KUYAMUDU maisha yako vizuri, Kwa sababu mianga ndiyo ina yo ashiria SIKU, MAJIRA na MWAKA wako. Je! wewe unajua SIKU, MAJIRA na MWAKA wako. ? Mianga ndiyo inayo sababisha siku ya kuzaliwa kwako iwe yako na si ya Shangazi wala Mjomba wako, ndiyo iliyosababisha wewe umezaliwa wakati huo uliozaliwa. Hivyo mianga ina nafasi kubwa sana juu ya Maisha yako maana ndiyo imebeba SIKU, MAJIRA na MWAKA wako, sasa kama hujajua siku yako hutajua Majira yako na kama hujajua Majira yako hutakaa UFAHAMU Mwaka wako. Matokeo yake unakuwa muhanga wa Siku, Majira na Mwaka, ...
MCHUNGAJI KIONGOZI - HUDUMA YA EFATHA RUVUMA, PHILIPO JAMES GUNI. SOMO: KUKUBALI. Tunahitaji kusikia Neno la Kristo linalohubiriwa na Manabii, Mitume na Watumishi wote wa Mungu, na baada kusikia kuna hatua inayofuata nayo ni KUKUBALI. 2 Nyakati 20:20 “Wakaamka asubuhi na mapema, wakaenda nje katika jangwa la Tekoa; nao walipokuwa wakitoka, Yehoshafati akasimama, akasema, Nisikieni, enyi Yuda nanyi wenyeji wa Yerusalemu; mwamini Bwana, MUNGU wenu, ndivyo mtakavyothibitika waaminini MANABII wake, ndivyo mtakavyo fanikiwa.” Unahitajika KUKUBALI yale yote yanayohusiana na Ufalme wa Mungu, kwa sababu Mungu ana mpango wa KUKUTHIBITISHA. Mafanikio hayaji kama Mungu HAJAYAPITISHA, Mibaraka haimfikii mtu yeyote tu isipokuwa yule ambaye Mungu amemuwekea MUHURI wake ya kwamba huyo ABARIKIWE. Mimi na wewe tunapaswa kukubali ya kwamba yule aliyetuwekea Ahadi nyingi katika Maisha yetu anataka KUZITHIBITISHA kwetu lakini YEYE Atazithibitisha kwa yule ambaye AMESIKIA NENO lak...
Image
ZIARA YA KITUME NA KINABII VISIWANI ZANZIBAR. Haleluya,......... Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akihojiwa na Vyombo mbalimbali vya Habari vya Zanzibar Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar baada ya Kuwasili Nchini humo.
Image
Naibariki Alhamisi yangu, Alhamisi yangu IMEBARIKIWA, Nami NIMEBARIKIWA, Nitayaweza YOTE katika YEYE Anitiaye NGUVU, Hakuna la KUNISHINDA, Ndani ya Mbawa zake Napata Kimbilio, Haleluya, MUNGU BABA Ni MZURI, Haleluya.
Image
Kama huwezi KUUKOMBOA wakati kwa kutumia muda wako mwingi kujifunza ulichofundishwa Kanisani, ibilisi atachukua nafasi katika maisha yako. Mtu yeyote anayeweza kusimama imara bila kumpa ibilisi nafasi, mtu huyo ni imara kwenye IMANI yake. Mtu huyu maongezi Yake yana nguvu na ni mtenda miujiza, watu wa aina hii walikuwa wamechoka lakini kwa sababu Ya IMANI waliyonayo wanakuwa imara, Hawalii ovyo, bali wanampa ibilisi wakati mgumu. WAAMINI ni wanajeshi wa jeshi la MUNGU hivy o hawaitaji kuonewa HURUMA . Kabla hujawa mwanajeshi lazima ujaribiwe kama unakidhi vigezo, hivyo usiogope kujaribiwa. Wakristo lazima wawe IMARA na NGUVU na UJASIRI mwingi. Jifunze kuwa mwanajeshi shupavu na usiruhusu ibilisi akuchezee chezee. Huwezi kumuweka ibilisi kwenye nafasi yake kama wewe mwenyewe hauko kwenye NAFASI YAKO . Ibilisi anakusukuma kwa sababu haupo kwenye nafasi yako, ukiamua kukaa kwenye nafasi yako ibilisi hataweza kukuonea tena. Wafilipi 2:13 " Kwa maana ndiye M...
Image
Naibariki Jumatano yangu, Jumatano yangu IMEBARIKIWA kama ilivyoamriwa na BWANA, Nitaishi kwa AKILI NZURI, Nitatenda KIFALME, Hakuna cha Kunizuia, ROHO YA BWANA Yu Juu Yangu, Haleluya, FURAHA Iko Nami, Haleluya, YESU Nakupenda, Asante BWANA.
Image
ZIARA YA KITUME NA KINABII - ZANZIBAR; PICHANI; Waimbaji wa Efatha Ministry Mass Choir walipokuwa wakiwasili Zanzibar kwa ajili ya Ziara ya Kitume na Kinabii, inayoanza hii leo Efatha Ministry Zanzibar.
Image
ZIARA YA KITUME NA KINABII MKOA WA DODOMA. SOMO: NEEMA YA MUNGU. NEEMA ni ya MUHIMU sana katika Maisha yako. Ni NEEMA tu ndiyo inayokupa wewe kupewa ZAWADI ambazo zitakufanya utoke katika Uhitaji na kufika mahali kwenye Utele. Ayubu 42:10 “Kisha BWANA akaugeuza uteka wa Ayubu, hapo alipowaombea rafiki zake; BWANA naye akampa Ayubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kwanza.” Neema inakujia pindi pale UNAPOTANGULIZA WENGINE unapo OMBEA na KUHESHIMU Maisha ya WENGINE Mungu anafurahi. Unapotatua matatizo ya wengine, Mungu anaona hayo maana YEYE anayafurahia hivyo inakuwa ni sawa na unajiandaa kupokea NEEMA. Ayubu 42:11-13 “Ndipo wakamwendea nduguze wote, waume kwa wake, nao wote waliojuana naye hapo zamani, wakala chakula pamoja naye katika nyumba yake; nao wakamlilia na kumtuza moyo katika habari za huo uovu wote BWANA aliouleta juu yake; kila mtu akampa kipande cha fedha, na pete ya dhahabu kila mmoja. Basi hivyo BWANA akaubarikia huo mwisho wa Ayubu zaidi ya m...