Kama huwezi KUUKOMBOA wakati kwa kutumia muda wako mwingi kujifunza ulichofundishwa Kanisani, ibilisi atachukua nafasi katika maisha yako. Mtu yeyote anayeweza kusimama imara bila kumpa ibilisi nafasi, mtu huyo ni imara kwenye IMANI yake. Mtu huyu maongezi Yake yana nguvu na ni mtenda miujiza, watu wa aina hii walikuwa wamechoka lakini kwa sababu Ya IMANI waliyonayo wanakuwa imara, Hawalii ovyo, bali wanampa ibilisi wakati mgumu.
WAAMINI ni wanajeshi wa jeshi la MUNGU hivyo hawaitaji kuonewa HURUMA . Kabla hujawa mwanajeshi lazima ujaribiwe kama unakidhi vigezo, hivyo usiogope kujaribiwa. Wakristo lazima wawe IMARA na NGUVU na UJASIRI mwingi. Jifunze kuwa mwanajeshi shupavu na usiruhusu ibilisi akuchezee chezee.
Huwezi kumuweka ibilisi kwenye nafasi yake kama wewe mwenyewe hauko kwenye NAFASI YAKO . Ibilisi anakusukuma kwa sababu haupo kwenye nafasi yako, ukiamua kukaa kwenye nafasi yako ibilisi hataweza kukuonea tena.
Wafilipi 2:13 " Kwa maana ndiye Mungu atendaye Kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema".
Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira -Efatha Ministry.

Comments