MCHUNGAJI KIONGOZI - HUDUMA YA EFATHA RUVUMA, PHILIPO JAMES GUNI.
SOMO: KUKUBALI.
Tunahitaji kusikia Neno la Kristo linalohubiriwa na Manabii, Mitume na Watumishi wote wa Mungu, na baada kusikia kuna hatua inayofuata nayo ni KUKUBALI.

2 Nyakati 20:20
“Wakaamka asubuhi na mapema, wakaenda nje katika jangwa la Tekoa; nao
walipokuwa wakitoka, Yehoshafati akasimama, akasema, Nisikieni, enyi
Yuda nanyi wenyeji wa Yerusalemu; mwamini Bwana, MUNGU wenu, ndivyo
mtakavyothibitika waaminini MANABII wake, ndivyo mtakavyo fanikiwa.”
Unahitajika KUKUBALI yale yote yanayohusiana na Ufalme wa Mungu, kwa sababu Mungu ana mpango wa KUKUTHIBITISHA. Mafanikio hayaji kama Mungu HAJAYAPITISHA, Mibaraka haimfikii mtu yeyote tu isipokuwa yule ambaye Mungu amemuwekea MUHURI wake ya kwamba huyo ABARIKIWE.
Mimi na wewe tunapaswa kukubali ya kwamba yule aliyetuwekea Ahadi nyingi katika Maisha yetu anataka KUZITHIBITISHA kwetu lakini YEYE Atazithibitisha kwa yule ambaye AMESIKIA NENO lake na KUKUBALI kile alicho KISIKIA, mtu huyo ukawe ni wewe kwa jina la YESU, Amen; UKATHIBITISHE KUPITIA NENO HILI.
Kwa nini unatakiwa Kukubali Habari za Ufalme wa Mungu unao hubiriwa? Kwa sababu unahitajika kuyabeba Mafanikio ya Ufalme wa Mungu.
Katikati ya watu wanao mtambulisha Mungu huku duniani wenye kuyabeba MAFANIKIO ni watu wachache sana. Kwa nini? Kwa sababu wengine WAMESIKIA lakini wamegoma kukubaliana na kile ambacho WAMEKISIKIA, hivyo hawawezi kupokea AHADI ambazo Mungu ameziahidi katika Maisha yao.
MUNGU akakujalie wewe kukubali kwa sababu YEYE Amekupa kuyabeba MAFANIKIO katika UFALME wake.
:- Mchungaji Kiongozi Philipo James Guni, EFATHA MINISTRY- RUVUMA.

Comments
Post a Comment