UKO TAYARI KUBADILISHA MUELEKEO WA KILE ULICHOKISIKIA: (Sehemu ya Nne).
Tumia MUDA wako mwingi katika kile ambacho unataka KIKUPE FAIDA, chukua Kalamu na Daftari, Haleluya, Chukua Kalamu na Daftari uwe una CHORA kila saa Muundo wa Serikali yako ya Kampuni, Muundo wa Utendaji, Namna utakavyoendesha Biashara zako, Unaandika kwenye Daftari lako, unalifunga, unaliweka Pembeni, Unakaa baada ya Miezi miwili tena, unachukua Daftari lingine, UNAPANGA tena, Unakumbuka Vizuri au Utakuwa umesahau, Unarudia tena, Unaweka pembeni, unakaa tena Mwezi mwingine, UNAUMBA tena, mpaka Unaona KWELI SASA kila kitu KIMEKAA.
:- Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Mwenge Dar es Salaam, Tanzania, EFATHA MINISTRY.
Comments
Post a Comment