UKO TAYARI KUBADILISHA MUELEKEO WA KILE ULICHOKISIKIA: (Sehemu ya Pili).
KATAKAA na UZIFUTE kwenye AKLI YAKO na UFAHAMU WAKO Habari zote ulizowahi Kuzisikia au Utakazozisikia au Unazozisikia zinazoonyesha KUSHINDWA au UHARIBIFU; nina maanisha Nini hapo? USIKUBALI KUMSIKILIZA Mtu anayesema …. “mmmh Unajua Mimi niliolewaga, eeeh…. Mmh yule Mwanaume balaaa, Nikaondoka mwenyewe….” Ukikaa naye huyo Mtu, na WEWE UTAONDOKA katika Ndoa yako, UKIMSIKILIZA huyo Mtu….. Na WEWE UTAONDOKA katika NDOA yako, na Kama hujaolewa…Hutakaa UOLEWE.
We Ukimuona tu anaanza KUKUAMBIA, … “Mwenzangu usinione hivi Niliolewaga miye” … Uliolewa? Eeeenh… “Mmmh Sasa hivi tuliachanaga” ….. Mliachana eeenhh? MUNGU Akubariki KWAHERI, …. MUAGE Mapema UENDE Zako USIMSIKILIZE, maana lazima Ataumba UHARIBIFU kwako.
Ukiona Binti mwenzio au Mkaka mwenzio, unamuuliza vipi Mbona Mjamzito Ndoa mmefunga lini?,…. Anakuambia “ aaah Ndio hivyo ilitokea tu, nilikuwa….” MKIMBIE, USISIKILIZE, UKIMSIKILIZA huyo Mtu na Wewe kama Hujaolewa au Hujaoa, Na WEWE UHARIBIFU huo huo UTAUMBIKA ndani yako.
YANAWAINGIA? YANAWAINGIA…… Hata kama ana UPAKO kama Josephat MKIMBIE, maana lazima ATAUMBA UHARIBIFU kwako, IMANI chanzo chake ni KUSIKIA.
:- Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.
Comments
Post a Comment