SOMO: SALA YA BWANA.
MAPENZI ya Mungu ni nini? Mapenzi yake ni wewe utende Mema. Wafilipi 4:8-9” Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo.” Yale mambo Unayofanya yataweza kumsababisha Mungu aje akae ndani yako au kumuweka mbali na wewe. Wewe unataka nini? Mungu afanye makao kwako au aondoke ? Nia yako wewe ni nini?
Kama hamna KWELI katika kitu au jambo ufanyalo hilo jambo achana nalo. Kama upo na watu ambao hawana KWELI ndani yao achana nao, kama unataka Mungu awe na wewe. Danieli na wenzake walipopewa chakula kizuri cha Mfalme walijua kuwa katika chakula hicho hakukuwa na KWELI ndani yake, hivyo wakaamua kuachana nacho na wakakataa kula na wakala chakula cha kienyeji kabisa na wakawa na Nguvu na akili kuliko wenzao. Chochote ambacho unaona kuwa HAKINA KWELI ndani yake usikifanye maana utamkosea Mungu.
Kama unataka kumuona Mungu katika maisha yako hakikisha lolote lile la KWELI unalifanya, ila ambalo si la kweli usifanye.
Kama unataka kumuona Mungu katika maisha yako hakikisha lolote lile la KWELI unalifanya, ila ambalo si la kweli usifanye.
Unapaswa kuwa makini na chakula unachokula, kwani kinaweza kuharibu akili yako, ubongo wako, mishipa yako na hata mzunguko wa damu katika mwili wako, hivyo mambo yoyote yaliyo ya kweli, hayo yafanye kwa uaminifu, usile kila kitu, usiweke ndani ya mwili wako kila kitu kwa maana kinaweza kuharibu maisha yako.
:- Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.
Comments
Post a Comment