ZIARA YA KITUME NA KINABII MKOA WA DODOMA.
SOMO: NEEMA YA MUNGU.
NEEMA ni ya MUHIMU sana katika Maisha yako. Ni NEEMA tu ndiyo inayokupa wewe kupewa ZAWADI ambazo zitakufanya utoke katika Uhitaji na kufika mahali kwenye Utele.
Ayubu 42:10 “Kisha BWANA akaugeuza uteka wa Ayubu, hapo alipowaombea rafiki zake; BWANA naye akampa Ayubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kwanza.”
Neema inakujia pindi pale UNAPOTANGULIZA WENGINE unapo OMBEA na KUHESHIMU Maisha ya WENGINE Mungu anafurahi. Unapotatua matatizo ya wengine, Mungu anaona hayo maana YEYE anayafurahia hivyo inakuwa ni sawa na unajiandaa kupokea NEEMA.

Ayubu 42:11-13 “Ndipo wakamwendea nduguze wote, waume kwa wake, nao wote waliojuana naye hapo zamani, wakala chakula pamoja naye katika nyumba yake; nao wakamlilia na kumtuza moyo katika habari za huo uovu wote BWANA aliouleta juu yake; kila mtu akampa kipande cha fedha, na pete ya dhahabu kila mmoja. Basi hivyo BWANA akaubarikia huo mwisho wa Ayubu zaidi ya mwanzo wake; ….” Neema ikikufikia unaletewa ZAWADI ambacho zitakufanya utoke kwenye umaskini na kukufikisha kwenye Utele.
Kwa nini unahitaji NEEMA? Ni kwa sababu umekwama hivyo ukiipata hiyo NEEMA inakukwamua. NEEMA ikikufikia hata kama ulikuwa na UGONJWA UNAPONA, matatizo yanaondoka na wale walio KUNYANYAPAA WANAKUJIA, walio KUKATAA WANAKUKUMBATIA na walio KUTEMA MATE WANAKUBUSU.
NEEMA ni ya MUHIMU sana katika Maisha yako, itamani usiku na mchana ili uweze kuipata.
MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA, EFATHA MINISTRY.

Comments

Popular posts from this blog

Mithali 8:17-21 "Nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia. Matunda yangu hupita dhahabu, naam, dhahabu safi, na faida yangu hupita fedha iliyo teule. Natembea katika njia ya haki, katikati ya mapito ya hukumu. Niwarithishe mali wale wanipendao, tena nipate kuzijaza hazina zao." Proverbs 8: 17-21 "I love them that love me; and those that seek me early shall find me. Riches and honour are with me; yea, durable riches and righteousness. My fruit is better than gold, yea, than fine gold; and my revenue than choice silver. I lead in the way of righteousness, in the midst of the paths of judgment: That I may cause those that love me to inherit substance; and I will fill their treasures."