ZIARA YA KITUME NA KINABII EFATHA MINISTRY – ZANZIBAR;
Ili uweze kuwa mshindi wa kesho yako ni lazima ujue Biblia inasemaje kuhusu hiyo kesho yako, Mwanzo 1:14 “Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya MCHANA na USIKU; nayo iwe ndiyo dalili na MAJIRA na SIKU na MIAKA;”
Biblia inasemaje kuhusu usiku na mchana? Kuna mianga iliyotenga kati ya Usiku na Mchana, Usipo kuwa na UFAHAMU utashindwa KUYAMUDU maisha yako vizuri, Kwa sababu mianga ndiyo inayo ashiria SIKU, MAJIRA na MWAKA wako.
Je! wewe unajua SIKU, MAJIRA na MWAKA wako. ?

Mianga ndiyo inayo sababisha siku ya kuzaliwa kwako iwe yako na si ya
Shangazi wala Mjomba wako, ndiyo iliyosababisha wewe umezaliwa wakati
huo uliozaliwa. Hivyo mianga ina nafasi kubwa sana juu ya Maisha yako
maana ndiyo imebeba SIKU, MAJIRA na MWAKA wako, sasa kama hujajua siku
yako hutajua Majira yako na kama hujajua Majira yako hutakaa UFAHAMU
Mwaka wako. Matokeo yake unakuwa muhanga wa Siku, Majira na Mwaka, na
hata Mwaka unaweza kuisha bila wewe hujafanya kitu chochote kile na wala
hujui huo Mwaka umeishaishaje maana unakuwa ni Msindikizaji tu wa
wengine ili waishi.
Kuna watu wanaishi hawajui hata kesho yao itakuwaje, wanaishi wakimshukuru Mungu tu, wanabaki kusema “Mwaka huu Mungu atanionekania” kwa lipi? Hajui nini kinakwenda kutokea kwake. Siku utakapojua SIKU, MAJIRA na MWAKA wako ndipo utaanza kujulikana wewe ni nani, kwa maana huo ndiyo UTAMBULISHO wako.
Ili uweze kufika mahali Ulipokusudiwa au Uweze kupokea BARAKA zako kutoka kwa Mungu ni lazima ujue SIKU yako ni ipi, MAJIRA yako na MWAKA wako pia.
MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA, EFATHA MINISTRY.

Comments
Post a Comment