SOMO: NGUVU YA MEMA NA MABAYA.
Ziko NGUVU mbili ambazo zinafanya Kazi katika ulimwengu wa Roho, hizi NGUVU mbili zinavutana kila iitwapo leo Nazo ni.
 - Nguvu ya MEMA na 
 - Nguvu ya MABAYA
Nguvu hizi haziwezi kuonekana kwa macho lakini tunaziona kupitia MATENDO ya mtu. Kuna MATENDO yakifanyika unapata kujua haya ni ya Roho MBAYA au Roho NZURI, yale ya Roho nzuri ni yale yaliyotendwa katika ROHO MTAKATIFU, yale ya roho mbaya yametendwa katika yule roho mchafu. Tunaweza ku baini NGUVU ya MEMA na MABAYA kupitia matendo ya mtu kwa sababu hatuwezi kuziona hizi roho mbili kwa macho ya kawaida. Kuna mtu akiona watu wanagombana anasikia kuumia, lakini kuna mwingine anafurahi watu wanapogombana, hivyo unajua tu ni Roho gani anayetenda kazi ndani yake.
Mungu ni Roho na ni Mtakatifu sana hivyo amua kuwa Mtakatifu kama YEYE ili uweze kutenda Matendo MEMA maana pasipo huo Utakatifu hatutaweza kumpendeza MUNGU.
:- Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira -EFATHA MINISTRY.

Comments