HALELUYA, HALELUYA, HALELUYA Kusanyiko TAKATIFU la Mwaka huu 2017 wa Kujibiwa MAOMBI Linakaribia. Kusanyiko litaanza tarehe 2/October - 8/ October, Kibaha Precious Centre Mji wa BWANA.
Kwa Wale ambao ni Wageni (Si Wana Efatha Ndani ya Tanzania na Nje ya Tanzania) na wengependa kuja KUPOKEA kile ambacho BABA YETU KIPENZI WA MBINGUNI Alichoandaa kupitia Wapakwa Mafuta wake wakiongozwa na Mtumishi wake Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, unapaswa KUJIANDIKISHA (REGISTER YOUR DETAILS) kupitia Website ya Huduma ambayo ni www.efathaministry.org kwa ajili ya Maandalizi ya Nafasi yako ya HOTEL (Malazi na Chakula) na kama pia utakuja na kuondoka (yaani hutalala) pia unapaswa KUJIANDIKISHA kwa ajili ya Utaratibu wa USAFIRI.
Mwisho wa Kujiandikisha ni tarehe 22/ September Mwezi huu.
Ukisha JIANDIKISHA utapokea E-mail yenye maelezo yote, pia unaweza kupata Maelezo yote katika Website yetu ya Huduma.
UBARIKIWE Mwana wa Mungu, YESU Anakupenda, YESU Anakujali.
"SHARE IT"...... na Mkaribishe na Mwenzio (Mke wako, Mume wako, Wazazi wako, Ndugu zako, Jirani zako, Wafanyakazi wenzio, Wanafunzi wenzako, Wafanyabiashara wenzako n.k.) na wale wooote ambao bado hawajampokea Bwana wetu YESU KRISTO kama BWANA na MWOKOZI wa Maisha yao, na Wooooote wenye Mapenzi Mema.
KARIBU, tunakusubiri Kukuona, KARIBU.
Comments
Post a Comment