Posts

Showing posts from August, 2016

PICHANI: Watumishi wa MUNGU wakimwadhimisha MUNGU kwenye Ibada ya pili kanisani Efatha Ministry mwenge Dar es salaam

Image

MCHUNGAJI FRIDA MNYANGI SOMO: UTAYARI WA KUTEMBEA NA MUNGU Safari ya kutembea na Mungu huanza pale ambapo mtu huamua kuokoka maana kuokoka niagizo la msingi kwa wote wanaotakwa kwenda mbinguni. (Mark 16: 15). Tunaona watumishi wengi mfano Musa, Ibarabimu walikuwa na utii wa kwa Mungu. Huwezi kumtumikia Mungu kama huna utii. Yesu yupo tayari kutembea na watu walio tayari kumtii Mungu. Kumtii Mungu ni pamoja kuwasikiliza na kutenda yote unayoagizwa na watumishi wake, mfano Wachungaji, Maaskofu, Viongozi wa cell na wengineo. - Older ikitolewa usiulize maswali fanya kama ulivyo agizwa ndio Mungu anapenda kufanya kazi na wale wampendao - Unapotembea na Mungu unahitaji kuelewa mambo ya msingi ili uweze kupatana naye. Amosi 3: watu wawili wanaweza kutembea pamoja pasipokuwa wamepatana, ni kweli huwezi kutembea na Mungu kama hujapatana yale. Unapatana naye kwa kuhakikisha tabia na mwenendo wako uko sawasawa na Mungu anavyokutata uwe. - Mungu anawapenda wale wanao leta watu kuokoka, kushuhudia wengine unakua rafiki wa Yesu maana anasema nawapenda wale wanipendao na wanitafutao kwa bidii wataniona. - Kuna watu wanateseka na mateso Mengi na wanatamani mtu awaambie habari za Yesu lakini hawajapata lakini wewe ni kazi yako kumfikia huyo mtu uzae matunda ili yaweze kukaa. - Ukiwa tayari unaacha dhambi ni adui wa dhambi utayari - Unapoamua kutembea na Mungu lazima utakutana na hatari nyingi, kusemwa na kukatishwa tama Mateso yasije yakakutenganisha na Mungu, ukikata tama ukamchukia Mungu Yule aliye kutoa mbali - Daniel 3:10 – 20 Shadrack Meshaki na Abednego walikuwa wako tayali kumwabudu Mungu na Mungu aliwatetea na akawatoa kwenye tanuru la moto ndivyo Mungu anaenda kukutetea kama hawa vijana watatu. - Mungu hawezi kukuacha upotee na wale wanao potea. Usije ukaicheze a hii neema Mungu atakutete Mungu wako iwe usiku jioni mchana na wajue ni Mungu gani unaye mwabudu.

Image

Efatha Ministry Mass choir wakimsifu Mungu kwenye Ibada ya Kwanza na Ibada ya Pili ambayo inaendela hapa Kanisani Efatha Ministry Mwenge, Dar es Salaam- Tanzania.

Image

Halleluya wana wa Mungu hili ni vazi maalumu kwa ajili ya kusanyiko kuu ambalo litafanyika mwezi wa kumi Precious Center Kibaha.

Image
Add caption
Image
MCHUNGAJI MARGRETH ILOMO SOMO: UTAYARI Efeso 6:13-17 “Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; …………” Utayari ni nini? ... See More
Image
MCHUNGAJI MARGRETH ILOMO SOMO: UTAYARI UTAYARI WA KUSOMA NENO LA MUNGU:- Wokovu wako unatakiwa kujilinda yaani kwa kusoma neno la Mungu maana hilo neno ni ulinzi tosha, na neno hilo ndio sindano tosha ya ile dhambi inayo kuzingwa kwa upesi katika maisha yako. ... See More

MCHUNGAJI MARGRETH ILOMO SOMO: UTAYARI Katika maisha yako usifanye jambo ili mwanadamu akuone maana watakuchelewesha fanya jambo ili Mungu akuone. Kila mtu aliyeumbwa na Mungu anakusudi la Mungu ndani yake hivyo fanya katika kusudi la Mungu alilo kuwekea maana ndani ya utumishi wako ndiko kwenye kila kitu unacho kihitaji katika maisha yako.

Image

MCHUNGAJI: ADELLAILA LUIZA SOMO: MOYO WA SIFA Mungu ni mwenye uweza haijalishi unapitia katika kitu gani iwe ni maumivu ya aina gani furahi maana anakupenda, unatakiwa ufurahi maana hii ni moja ya shukrani yako kwake. Filipi 4:4 “Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini. ” Unapofurahi unasukuma magonjwa mbali na wewe na adui yako anakimbia mbele yako. Kufurahi kwako siku zote adui yako anakuwa mdogo kuliko sisimizi, unapokuwa na huzuni adi yako ndio anafurahi bali furaha ya Mungu ni kukuona unafurahi. UTAMJUAJE MTU MWENYE MOYO WA SIFA AU WA SHUKRANI 1. Anakuwa na furaha wakati wote, mtu wa aina hii siyo kwamba hana ambayo anayopita nayo hapana lakini ana moyo wa shukrani mbele za Mungu, ukifurahi mbele za Mungu hatakama unamagonjwa yanaponywa na furaha yako itakufanya uwe na Mungu kila wakati. 2. Mtu mwenye moyo wa sifa anakuwa na shukrani, Mungu akiona una moyo wa shukrani anakupa kila kitu unacho kihitaji. 3. Mtu mwenye moyo wa shukrani anakuwa na UPENDO wa kujipenda mwenyewe na wakupenda wengine. 1korintho 13:4-8 “Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu. Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;……….. ” mtu anayependa wengine hawezi kuwaona wanalia halafu akanyamaza balia anawahurumia na kuwasaidia. 4. Mtu mwenye moyo wa sifa wakati wote anasimulia matendo ya Mungu, 5. Mtu mwenye moyo wa sifa hana manung’uniko wakati wote anashukuru katika kila jambo.

Image

Kwaya ya vijana waimbaji chipkizi Efatha wakiongoza Ibada ya tatu kumsifu na kumuabudu MUNGU. Hakika SIFA NA UTUKUFU zina MUNGU.

Image

KILA JAMBO NA WAKATI WAKE. Leo ni siku muhimu sana kwa ndugu zetu hawa, ambao leo wameamua kuyatoa maisha yao kwa BWANA YESU ili awe Bwana na Mwokozi wa maisha yao. NEEMA ya MUNGU iwe nanyi iwatunze asiwepo atayerudi nyuma. MTAKUWA WATU WAKUU, Wengi wataokolewa kupitia ninyi.

Image

PICHANI: Mama Eliyakunda Mwingira akisalimia kanisa katika Ibada ya kwanza na kutoa salamu kutoka kwa Baba yetu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, ambaye yupo mikoani katika kuifanya kazi ya Mungu.

Image

MCH. FRIDA MNYANGI SOMO : NGUVU YA UPENDO Mungu ni pendo ukiwa na nguvu ya upendo inasababisha kuwa na huruma huta mkanyaga jirani (Yohana 3:16-17 " Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.") Japo tulikuwa na dhambi, MUNGU alitusamehe hata kabla ya kumwomba, na sisi tunatakiwa kuwasamehe waliotukosea hata kama hawajaomba msamaha. Upendo unaanzia kwa mkeo ama Mumeo na kwa watoto na kwajirani yako kwani hainamaana kwamba unampenda Mungu wakati Mumeo mkeo humpendi. Hata kama jirani yako amekusengenya mpende tu usimshikilie mtu ndani ya moyo wako, Hata ukinenewa mabaya potezea futa kabisa ili uweze kuiona mbingu. Ukimpenda Mungu lazima umpende na jirani yako aliye umbwa kwa sura ya Mungu (1Yohana 4:19-20 "Mtu akisema anampenda Mungu naye akimchukia ndugu yake ni mwongo, asiye mpenda ndugu yake ambaye hakumuona hawezi kumpenda Mungu asiye Mwona"). - Nguvu ya upendo inasabababisha unakuwa na msamaha - Inasababisha kumpenda mtu hata kama anakufanyia mabaya ikiwa ndani yako utamsamehe bila yeye kuomba msamaha

Image

PICHANI: Efatha Mass choir wakimsifu na kumwabudu MUNGU WETU MKUU kwenye Ibada ya pili inayoendelea hapa Efatha Mwenge Dar es salaam

Image

Mchungaji Margareth Ilomo: WAOMBEE WANAOKUUDHI ILI UWE MKAMILIFU: Ukiwaombea wanaokuudhi na kuwatangazia msamaha ni injili tosha, Mtu akikuudhi nenda kamnunulie zawadi nzuri na umpelekee, ile zawadi itamfanya akupende na wakati mwingine atakutete akisikia mtu anakusema vibaya atasema yule hapana hayuko hivyo. Je ulisha wahi kumnunulia zawadi mtu aliyekuudhi? Fanya hivyo na utamwona MUNGU katika maisha yako. 2 Timotheo 3:12 "Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa, lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika."

Image

Mchungaji Margareth Ilomo: WAOMBEE WANAOKUUDHI ILI UWE MKAMILIFU: Mathayo 5:43-48" Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako; lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki......" MUNGU hapendi KISASI NA KINYONGO kwasababu kisasi na kinyongo kitakumaliza wewe mwenyewe, na utakufa mapema kwa Presha na kisukari. Maudhi hayatoki kwa mtu wa mbali bali yanatoka kwa watu wanaokuzunguka kama Mume, mke, shemeji, kazini kwako na kadhalika na huo ndio uwanja wa ibilisi wa kufanyia kazi zake. Wewe uliyeokoka unatakiwa kujilinda, kaa katika wokovu kwa malengo na adui hatakupata.

Image

SHUHUDA Naitwa Mboni Mwaminifu namshukuru Mungu kwa Kumkomboa na Kumponya mwanangu kutoka katika nguvu za kichawi. Shetani alimtumia kuharibu vitu vingi na kufanya mambo mengi ya kipepo, tulihangaika makanisa mengi bila kupata msaada, lakini siku moja tukaamua kumleta hapa Efatha ambapo aliombewa na siku ya tarehe 14/8/2016 tulienda Precious Center Kibaha ambapo kulikuwa na Ibada, Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira alitamka kuwa kila uchawi na ulozi mwisho leo, na tukashiriki meza ya Bwana baada ya Ibada ile alitapika sana na sasa amekuwa mzima kwa kuwa amefunguliwa kutoka katika nguvu hizo ambazo alipewa na Bibi yake. Hakika Mungu ni mkuu na anatenda mambo ya ajabu Sifa na Utukufu namrudishia yeye aliye mwenye uweza wote.

Image

Karibuni sana katika ibada nzuri za Jumapili ya 21/8/2016 hapa Efatha Ministry Mwenge Dar es salaam Tanzania, ibada ya kwanza inaendelea kwa wewe uliye njiani au nyumbani tunazo ibada tatu siku ya Jumapili. RATIBA ZA IBADA JUMAPILI - Ibada ya Kwanza; saa 1:00 - 4:00 Asubuhi - Ibada ya Pili; saa 4:00 - 7:00 Mchana - Ibada ya Tatu; saa 7:00 - 10:00 Jion

Karibuni sana katika ibada nzuri za Jumapili ya 21/8/2016 hapa Efatha Ministry Mwenge Dar es salaam Tanzania. Ibada ya kwanza inaendelea, kwa wale walioko mbali na Efatha Ministy mnaweza kufuatilia ibada za siku ya leo kupitia ukurasa huu wa facebook, online radio www.mixlr.com/efatha-ministry.

PICHANI: Mtumishi wa Mungu mama Eliyakunda Mwingira, akifungua Ibada ya leo.

Image

MAMA ELIAKUNDA MWINGIRA: Warumi 12:6- 21” Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani; ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake;........” Kila mmoja amepewa kipawa chake na Mungu, kila aliyenacho anatakiwa kukitendea kazi sawasawa na vile alivyopewa na kufanya kwa bidii na sio kwa ulegevu, usimlipe mtu ovu kwa ovu au ubaya kwa ubaya bali ufanye kila jambo kwa kuonyesha UTUKUFU kwa MUNGU. Katika kila kipawa ulichopewa fanya kwa bidii kwa kuwa hujajipa wewe mwenyewe bali yuko aliyekupa. Kila ufanyalo ufanye kwa UTAKATIFU kwa kuwa hakuna aliyebora kuliko mwingine wala usijihesabie haki. Katika yoote tuyafanyayo tukipendana sisi kwa sisi tutaushinda ubaya. Mungu peke yake ndiye anastahili kuhukumu kwa kuwa Mungu hayuko kwa ajili ya ubaya ila kwa UPENDO usihukumu kwa kuwa jukumu hilo ni la Mungu peke yake.

Image
Image
MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA: Katika Ibada ya leo hapa Precious Center Kibaha.
Image
PICHA kutoka Ibadani Efatha Ministry - Precious Center Kibaha Pwani, ambapo Ibada ya kupokea vipawa na kufufua vipawa vya Roho Mtakatifu. Nawe unayetufuatilia kaa tayari kupokea au kufufuliwa kipawa chako.

MCHUNGAJI ZEBEDAYO SANGA Kipawa ni nini? Ni Uwezo anaopewa mtu ili aweze kutenda kazi, hivyo kipawa ni kitendea kazi, Mungu napokupa kipawa maana yake amekupa majukumu kwani kipawa ni kwa ajili ya majukumu ya kufanya kazi aliyokupa Mungu. Watu wengi hawafanyii kazi kipawa bali wanataka Neema na bila kujua kuwa hiyo Neema haiji bila kukifanyia kazi kipawa. Neema ni nini? Neema ni kupata kitu bila kukitaabikia,unapo kitendea kazi hicho kipawa ndipo Mungu anakupa neema yake kwa kuwa wapo wale ambao wanamhitaji Mungu nao wanatakiwa wapitie kwako. Unaponyenyekea katika hiyo Neema ndipo mambo yote yanakuwa safi na unapochochea kipawa chako ndipo Neema inaongezeka. Na unapochochea kipawa ulichonacho wengi watakusema na wanapokusema hawakusemi wewe bali wanamsema aliyekupa hicho kipawa kwa maana kazi sio ya kwako ila ni ya Bwana naye atashughulika nao, na kinachotakiwa ni kuchochea karama, na usiwe mtu wa kujiinua pale Mungu anapokutumia. Wafilipi 3:12 “Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu.”

Mch Daniel Njuguna KAZI YA VIPAWA 1. Nikushughulikia WATAKATIFU yaani wateule 2. Kujenga WATAKATIFU waufikie uteule wao 3. Kuujenga mwili wa Kristo ili kuijenga Imani 4. Kipawa lazima kiongezeke kutoka daraja hadi daraja Mtu aliyepokea kipawa chake na kukitunza huwa hayumbishwi kwa kitu chochote. Efeso 2:8-10 “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.” Yapo mambo ambayo Mungu aliyatengeneza ndani yetu lakini hatuyajui hiyo ndio inapelekea wengi kupoteza hicho kitu, utakapotambua kuwa unakipawa na unakitendea kazi ndipo kipawa hicho kitakapofanya kazi ndani yako.

Image
Image
MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA: Pasipo kipawa tarajio la moyo linapotea kwasababu kipawa hakipo kwenye nafasi yake. Mfano:- Kuna mtu anatarajia ndoa nzuri, biashara nzuri lakini kipawa kisipochukua nafasi yake huwezi kufikia tarajio lako. Kipawa ndio uhai wako, kipawa kikianza kazi hata meno hayang'oki ovyo, kipawa kinakufanya uwe salama. Wengine wanafikiri kipawa ni kitu kidogo HAPANA, kipawa ndio uhai wako.