MCHUNGAJI FRIDA MNYANGI SOMO: UTAYARI WA KUTEMBEA NA MUNGU Safari ya kutembea na Mungu huanza pale ambapo mtu huamua kuokoka maana kuokoka niagizo la msingi kwa wote wanaotakwa kwenda mbinguni. (Mark 16: 15). Tunaona watumishi wengi mfano Musa, Ibarabimu walikuwa na utii wa kwa Mungu. Huwezi kumtumikia Mungu kama huna utii. Yesu yupo tayari kutembea na watu walio tayari kumtii Mungu. Kumtii Mungu ni pamoja kuwasikiliza na kutenda yote unayoagizwa na watumishi wake, mfano Wachungaji, Maaskofu, Viongozi wa cell na wengineo. - Older ikitolewa usiulize maswali fanya kama ulivyo agizwa ndio Mungu anapenda kufanya kazi na wale wampendao - Unapotembea na Mungu unahitaji kuelewa mambo ya msingi ili uweze kupatana naye. Amosi 3: watu wawili wanaweza kutembea pamoja pasipokuwa wamepatana, ni kweli huwezi kutembea na Mungu kama hujapatana yale. Unapatana naye kwa kuhakikisha tabia na mwenendo wako uko sawasawa na Mungu anavyokutata uwe. - Mungu anawapenda wale wanao leta watu kuokoka, kushuhudia wengine unakua rafiki wa Yesu maana anasema nawapenda wale wanipendao na wanitafutao kwa bidii wataniona. - Kuna watu wanateseka na mateso Mengi na wanatamani mtu awaambie habari za Yesu lakini hawajapata lakini wewe ni kazi yako kumfikia huyo mtu uzae matunda ili yaweze kukaa. - Ukiwa tayari unaacha dhambi ni adui wa dhambi utayari - Unapoamua kutembea na Mungu lazima utakutana na hatari nyingi, kusemwa na kukatishwa tama Mateso yasije yakakutenganisha na Mungu, ukikata tama ukamchukia Mungu Yule aliye kutoa mbali - Daniel 3:10 – 20 Shadrack Meshaki na Abednego walikuwa wako tayali kumwabudu Mungu na Mungu aliwatetea na akawatoa kwenye tanuru la moto ndivyo Mungu anaenda kukutetea kama hawa vijana watatu. - Mungu hawezi kukuacha upotee na wale wanao potea. Usije ukaicheze a hii neema Mungu atakutete Mungu wako iwe usiku jioni mchana na wajue ni Mungu gani unaye mwabudu.


Comments