MAMA ELIAKUNDA MWINGIRA: Warumi 12:6- 21” Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani; ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake;........” Kila mmoja amepewa kipawa chake na Mungu, kila aliyenacho anatakiwa kukitendea kazi sawasawa na vile alivyopewa na kufanya kwa bidii na sio kwa ulegevu, usimlipe mtu ovu kwa ovu au ubaya kwa ubaya bali ufanye kila jambo kwa kuonyesha UTUKUFU kwa MUNGU. Katika kila kipawa ulichopewa fanya kwa bidii kwa kuwa hujajipa wewe mwenyewe bali yuko aliyekupa. Kila ufanyalo ufanye kwa UTAKATIFU kwa kuwa hakuna aliyebora kuliko mwingine wala usijihesabie haki. Katika yoote tuyafanyayo tukipendana sisi kwa sisi tutaushinda ubaya. Mungu peke yake ndiye anastahili kuhukumu kwa kuwa Mungu hayuko kwa ajili ya ubaya ila kwa UPENDO usihukumu kwa kuwa jukumu hilo ni la Mungu peke yake.


Comments