SHUHUDA Naitwa Mboni Mwaminifu namshukuru Mungu kwa Kumkomboa na Kumponya mwanangu kutoka katika nguvu za kichawi. Shetani alimtumia kuharibu vitu vingi na kufanya mambo mengi ya kipepo, tulihangaika makanisa mengi bila kupata msaada, lakini siku moja tukaamua kumleta hapa Efatha ambapo aliombewa na siku ya tarehe 14/8/2016 tulienda Precious Center Kibaha ambapo kulikuwa na Ibada, Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira alitamka kuwa kila uchawi na ulozi mwisho leo, na tukashiriki meza ya Bwana baada ya Ibada ile alitapika sana na sasa amekuwa mzima kwa kuwa amefunguliwa kutoka katika nguvu hizo ambazo alipewa na Bibi yake. Hakika Mungu ni mkuu na anatenda mambo ya ajabu Sifa na Utukufu namrudishia yeye aliye mwenye uweza wote.

Comments