MCH. FRIDA MNYANGI SOMO : NGUVU YA UPENDO Mungu ni pendo ukiwa na nguvu ya upendo inasababisha kuwa na huruma huta mkanyaga jirani (Yohana 3:16-17 " Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.") Japo tulikuwa na dhambi, MUNGU alitusamehe hata kabla ya kumwomba, na sisi tunatakiwa kuwasamehe waliotukosea hata kama hawajaomba msamaha. Upendo unaanzia kwa mkeo ama Mumeo na kwa watoto na kwajirani yako kwani hainamaana kwamba unampenda Mungu wakati Mumeo mkeo humpendi. Hata kama jirani yako amekusengenya mpende tu usimshikilie mtu ndani ya moyo wako, Hata ukinenewa mabaya potezea futa kabisa ili uweze kuiona mbingu. Ukimpenda Mungu lazima umpende na jirani yako aliye umbwa kwa sura ya Mungu (1Yohana 4:19-20 "Mtu akisema anampenda Mungu naye akimchukia ndugu yake ni mwongo, asiye mpenda ndugu yake ambaye hakumuona hawezi kumpenda Mungu asiye Mwona"). - Nguvu ya upendo inasabababisha unakuwa na msamaha - Inasababisha kumpenda mtu hata kama anakufanyia mabaya ikiwa ndani yako utamsamehe bila yeye kuomba msamaha


Comments