MCHUNGAJI ZEBEDAYO SANGA Kipawa ni nini? Ni Uwezo anaopewa mtu ili aweze kutenda kazi, hivyo kipawa ni kitendea kazi, Mungu napokupa kipawa maana yake amekupa majukumu kwani kipawa ni kwa ajili ya majukumu ya kufanya kazi aliyokupa Mungu. Watu wengi hawafanyii kazi kipawa bali wanataka Neema na bila kujua kuwa hiyo Neema haiji bila kukifanyia kazi kipawa. Neema ni nini? Neema ni kupata kitu bila kukitaabikia,unapo kitendea kazi hicho kipawa ndipo Mungu anakupa neema yake kwa kuwa wapo wale ambao wanamhitaji Mungu nao wanatakiwa wapitie kwako. Unaponyenyekea katika hiyo Neema ndipo mambo yote yanakuwa safi na unapochochea kipawa chako ndipo Neema inaongezeka. Na unapochochea kipawa ulichonacho wengi watakusema na wanapokusema hawakusemi wewe bali wanamsema aliyekupa hicho kipawa kwa maana kazi sio ya kwako ila ni ya Bwana naye atashughulika nao, na kinachotakiwa ni kuchochea karama, na usiwe mtu wa kujiinua pale Mungu anapokutumia. Wafilipi 3:12 “Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu.”

Comments

Post a Comment