Mch Daniel Njuguna KAZI YA VIPAWA 1. Nikushughulikia WATAKATIFU yaani wateule 2. Kujenga WATAKATIFU waufikie uteule wao 3. Kuujenga mwili wa Kristo ili kuijenga Imani 4. Kipawa lazima kiongezeke kutoka daraja hadi daraja Mtu aliyepokea kipawa chake na kukitunza huwa hayumbishwi kwa kitu chochote. Efeso 2:8-10 “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.” Yapo mambo ambayo Mungu aliyatengeneza ndani yetu lakini hatuyajui hiyo ndio inapelekea wengi kupoteza hicho kitu, utakapotambua kuwa unakipawa na unakitendea kazi ndipo kipawa hicho kitakapofanya kazi ndani yako.

Comments