Mchungaji Margareth Ilomo: WAOMBEE WANAOKUUDHI ILI UWE MKAMILIFU: Mathayo 5:43-48" Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako; lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki......" MUNGU hapendi KISASI NA KINYONGO kwasababu kisasi na kinyongo kitakumaliza wewe mwenyewe, na utakufa mapema kwa Presha na kisukari. Maudhi hayatoki kwa mtu wa mbali bali yanatoka kwa watu wanaokuzunguka kama Mume, mke, shemeji, kazini kwako na kadhalika na huo ndio uwanja wa ibilisi wa kufanyia kazi zake. Wewe uliyeokoka unatakiwa kujilinda, kaa katika wokovu kwa malengo na adui hatakupata.

Comments