Mchungaji Margareth Ilomo: WAOMBEE WANAOKUUDHI ILI UWE MKAMILIFU: Ukiwaombea wanaokuudhi na kuwatangazia msamaha ni injili tosha, Mtu akikuudhi nenda kamnunulie zawadi nzuri na umpelekee, ile zawadi itamfanya akupende na wakati mwingine atakutete akisikia mtu anakusema vibaya atasema yule hapana hayuko hivyo. Je ulisha wahi kumnunulia zawadi mtu aliyekuudhi? Fanya hivyo na utamwona MUNGU katika maisha yako. 2 Timotheo 3:12 "Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa, lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika."

Comments