Posts
Showing posts from April, 2014
Darasani!
- Get link
- X
- Other Apps
"Watu wengi wameishi kwenye Wokovu kwa miaka mingi lakini maisha yao yamekuwa ni ya dhiki na kushindwa pamoja na kujifariji katika hali hizo. Wengi wamesimamia mafundisho na mapokeo ya aina aina lakini hawajasaidika. Safari ya kwenda mbinguni haiishi katika kuokoka tu bali inataka ifanyike kazi kubwa ili kumwandaa na kumkamilisha mtu hadi afikie cheo cha KRISTO. BWANA MUNGU akasema ni YEYE atufundishaye ili tupate faida. Faida ni pamoja na kufika MWISHO MWEMA wa Safari na sio Kufia njiani. Uzoefu wangu kwenye Utumishi wa BWANA wetu YESU KRISTO umeonyesha kuwa TABIA tulizo nazo zimechangia kwa kiasi kikubwa katika kutofanikiwa kwa Wana wa MUNGU. TABIA tulizo nazo mbali na mambo mengine zimetunyima: i) Kufanya IBADA na MUNGU wetu ambalo ndilo KUSUDI KUU la kuwepo kwetu chini ya jua. ii) Mafanikio na Baraka za Kiroho, Kiafya, Kiuchumi, Kindoa na Kimaisha. iii) Amani na MUNGU na Wanadamu pia. Tusipopona katika kurekebisha tabia zetu ni vigumu sana majina yetu kuandikwa katika k...
Ibada ya leo ilikuwa Nzuri sana Na Mtume na Nabii Josephat Erias Mwingira! Ametulisha neno kweli tumetolewa mahali,Muombe mungu azidi kumtumia mtumishi wake kwa ajili ya kazi ya Mungu anayo Ifanya, Unapoomba Mungu naye atafanya ya kwako kwa sababu ni mwaminifu Ameeen!
- Get link
- X
- Other Apps
Ni jumapili Nyingine tena watu wa mungu, tuende mbele za mungu wetu, kwa sifa na shukrani, tukimshukuru kwa wiki nzima yote, ametuongoza, ametulinda, na ametufanya tuione tena siku hii ya leo, amka na nyumba yako ukajumuike na Wana EFATHA Tanzania na Nje ya Nchi ukapate mbaraka wako USIKOSE mwana wa mungu mpendwa! Mungu akubariki sana!
- Get link
- X
- Other Apps
DARASA/CHUMBA CHA MAFUNDISHO: ''Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY. (Darasa linaendelea lilipoishia...) "Hebu angalia midomo yako imesema nini na nini? Umekiri nini na hujatimiza, umedanganya mbele ya MUNGU aliye HAI. Ni vizuri angalia hicho kinywa hakijaropoka chochote. Biblia inasema, “Mpende jirani yako kama nafsi yako”, hivyo kabla hujampenda mtu anza kujipenda mwenyewe. Kama wewe unateseka ni ngumu kumsaidia mwingine. Kama unahubiri Baraka, lazima tuzione hizo Baraka kwanza kwako ndipo tupokee na sisi. Ukidhamiria ndani ya moyo wako na kuyatendea kazi haya uyasomayo, YEYE ni wa KWELI na ATAKUWEZESHA kuijua KWELI na Ukishajua KWELI utakuwa HURU KWELI KWELI."" (Darasa linaendelea...)
- Get link
- X
- Other Apps
KESHO KESHO KESHO: Usikose Mwana wa MUNGU, Wewe Kijana, Mwanafunzi Usikose, Mahali: Diamond Jubilee Hall. TANZANIA INTELLECTUALS' SUMMIT 2014 Theme: The Role of Intellectuals in Advancing the Kingdom of God and cause positive changes in their societies. Venue: Diamond Jubilee Date: 26 th April 2014 Time: 14:00 - 20:00 hours Host: Apostle and Prophet Josephat E. Mwingira. Guest speakers: Mr. Paul Mashauri ( Businessman), Mr. John Ulanga - Founder of Foundation for Civil societies, Mr. Innocent Mungy (Head of corporate communications at Tanzania Communications Regulatory Authority), Dr. Askwar Hilonga - PhD holder of Science and a lecturer at Nelson Mandela Science and Technology Institute in Arusha and others... - Live performance by Efatha Intellectuals Band. - Get thru Mindset, Focus and Get started for Tanzania. Join with thousands for the birthing of great pioneers.
- Get link
- X
- Other Apps
DARASA/CHUMBA CHA MAFUNDISHO: ''Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY. (Darasa linaendelea lilipoishia...) Yakobo 4:6 “Lakini hutujalia sisi Neema iliyozidi, kwa hiyo husema Mungu huwapinga wajikwezao bali huwapa Neema wanyenyekevu”. Unaonaje wakati huu UJINYENYEKEZE kwa MUNGU wetu upitapo katika mambo magumu na mazito ili AKUKWEZE ili apate KUKUONYESHA njia ya kutokea na namna ya kuyashinda yanayokuzunguka. Adui wa mtu ni wa nyumbani mwake! Kagua nyumba yako sasa, jikague mwenyewe. Mfano:- Kuna Baba mmoja alisema mkewe hamfurahishi kabisa, lakini huyo mke ni wa kwako kama hajakufurahisha elewa kwamba hajafurahi. Maana hata anayesema hajashiba ni kwa sababu hajala. Tafuta kisababisho cha kumfurahisha mumeo. Katika hiyo nyumba iliyojengwa kuna wapangaji- kuna mikono, masikio, miguu, macho, n.k Lazima uangalie hiyo mikono yako imekupelekea kufanya nini? Hiyo miguu imekutembeza wapi na wapi? Ndiyo maana Biblia inasema tukae vitandani mwetu na kutulia na uitafakari sheria ya BWANA. Hebu tafakari tangu ulipozaliwa, mikono yako imefanya nini? Je umeungana na watu wasiomcha MUNGU? Je umewagawia mapato yako watu wanaokwenda kwa waganga wa kienyeji? Je hiyo miguu imekupeleka mahali pa uovu? TAFAKARI! Siyo kila sherehe unatakiwa uende; siyo kila kiti unatakiwa uweke makalio yako maana viti vingine vinawaka moto! Biblia imesema “Vikao vingine vya kifahari ni vya hila”. (Usikose Darasa, sasa ni wakati wa USHINDI)
- Get link
- X
- Other Apps
"Kubali kumtumikia MUNGU; Muabudu MUNGU hapigwi na adui, Muabudu MUNGU hasumbuliwi na adui, Muabudu MUNGU hakosi chakula. Mfanya Ibada analindwa, Mfanya Ibada anazungukwa. Akaniambia, ‘’Nimekupa Huduma ndani yako ya kuhamishia’’. Pia, wakati huo huo, alinifanyia vitu kadhaa. Aliyashika macho yangu, akatoa vigamba vigamba na kusema, ‘’Kuanzia sasa, utaona mambo ya Ki-Ungu. Mambo yaliyo katika ulimwengu wa roho’’. Akanishika mikono na kuambatanisha na mikono yake. Alipotoa mikono yake, nikaingalia mikono yangu nikaona damu. Akasema, ‘’Nimeitakasa mikono yako, ili kila utakalolifanya likafanikiwe, na kila utakayemwekea mikono, akafunguliwe’’. Kiisha kwenye macho akaweka Malaika, mmoja asimame upande huu na mwingine upande huu – walinde macho yangu usiku na mchana, ili kuweza kuona njia ya kwenda na kitu cha kufanya kwa ajili ya BWANA, na kwa ajili watu wake wanaokuja kwa ajili ya kumjua BWANA. Kisha akayagusa masikio yangu na kusema, ‘’Kuanzia sasa, utaisikia sauti yangu kwa usahihi’’. Kwenye kinywa, akanifanyia kitu cha ajabu sana! Akaweka kidole kinywani mwangu, akanigusa na kusema, ‘’KUanzia sasa, NENO limetakaswa kinywani mwako’’. Halafu akanishika miguu yangu katika sehemu ya magoti na akasema, ‘’Umetiwa nguvu miguuni na hata kwenye kiuno’’. Akaongeza kusema, “Utafanya kazi ambayo wengine hawajawahi kufanya’’. Baadae akasema, ‘’Kuanzia sasa, nimeweka mamlaka juu yako, na nguvu na uwezo’’. Akaniambia maneno mengi ya kunitamkia kwamba amenipa Huduma ya kuhamishia ya ‘Kitume’ na ‘Kinabii’. Akasema, “Katika Utume wako, mwangalie sana Paulo alivyopita kimamlaka, itafanana na hilo. Katika Unabii, angalia Isaya alivyotabiri. Utatabiri mambo yajayo mambo ambayo hayajawahi kuwepo bado, wala hayajawahi kutokea, wala hakuna aliyewahi kuyatamka katika kizazi chako na katika jamii yako, na yote yatatimia’’. Akaniambia , “Utaweza kuwahudumia Mitume, Manabii na wenye huduma zingine". : Apostle & Prophet Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.
- Get link
- X
- Other Apps
DARASA/CHUMBA CHA MAFUNDISHO: ''Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY. (Darasa linaendelea lilipoishia...) "Hapa ukifuatilia utajua adui za mtu ni wa nyumbani mwake mwenyewe; wakikasirika hawa ni wabaya sana maana wanakujua vizuri na wako jirani na wewe na wanakufikia kwa urahisi; hivyo kukuharibu ni rahisi sana. Na hao wanaokuharibu ndio wenyeji! Biblia inasema utoke katika hao jamaa zako ili MUNGU awe kwako BABA. Anapozungumzia awe BABA tena BABA MWENYEZI ana maana gani?, Ana maana YEYE ATAKUTUNZA kama mtoto wake nawe utakaa kwa SALAMA bila kitu kukutikisa wala kupungukiwa na kitu. Kama Neno lisemavyo: 2 Kor 6:1-10 “Nasi tukitenda kazi pamoja naye, twawasihi msiipokee Neema ya Mungu bure kwa maana asema hivi, wakati uliokubalika nalikusikia, siku ya Wokovu nalikusudia, tazama wakati uliokubalika ndio sasa; tazama siku ya wokovu ndiyo sasa. Tusiwe kwazo la namna yoyote katika jambo lolote, ili utumishi wetu usilaumiwe bali katika kila Neno tujipatie sifa njema; kama watumishi wa Mungu, katika saburi nyingi, dhiki, misiba, shida, vifungo, fitina, taabu, kukesha, kufunga, kuwa safi, elimu, utu wema; Roho Mtakatifu, upendo, neno la kweli; nguvu za Mungu, kwa silaha za haki za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto; kwa utukufu au kwa aibu; kwa kunenewa vibaya au vema kama wadanganyao bali tu watu wa kweli; kama wasiojulikana bali wajulikanao sana! Kama wanaokufa kumbe tu hai, kama wanaorudiwa bali wasiouawa; kama wenye huzuni bali siku zote tu wenye furaha; kama maskini bali tukijitajirisha na kuwatajirisha na wengine; kama wasio na kitu bali tu wenye vitu vyote”" (Usikose darasa mwana wa MUNGU, Neema hii ni yako sasa).
- Get link
- X
- Other Apps
TESTIMONT TESTIMONY TESTIMONY. "A child of GOD Jimmy Mhando, from Jerusalem region, Zone no 12 (Ubungo National Housing-Army Quarters), Decided to invite other zone members to Thank THE ALMIGHTY LOVELY GOD OF EFATHA Ministry for HIS Great Deeds. He began by saying, “I thank the GOD of Efatha, I thank JESUS of Efatha. I had a case in court that was not true. I was accused of stealing items worth Tshs.300, 000. The same person who opened the case in court for me is the same person that raided a plot belonging to my mother (My mother passed away suddenly at the Ubungo Bus Terminal. She fell as she was alighting from the bus and died on the spot). I was now tight with issues, one being I have been falsely accused of stealing and secondly, my mother death, thirdly this same man wants to grab my mother’s plot and possess it with its title deeds. I was really pressured in court that there is this one time when this man to me to Prison (Segerea Prison). This whole time I had not been born again. One day a man and a woman came and gave me the word of GOD and they also invited me to the Zone service. I went to the zone and I was prayed for; that very day I decided to accept Christ Jesus as my Lord and Saviour. From that time I involved my Bishop on the plight that I was facing. The Bishop and her husband began to pray for me; every time I used to go to court I told them so that they may pray for me. The GOD of Efatha is a doing GOD. I began to see changes; I started having peace in my heart. Then there came some people who would help me in the case of the man who wanted to take our plot falsely. He also threatened me saying he would show me because he had the money. But this JESUS of Efatha is able. People came and began to help me in law, and I did not even know them. The truth is that I am amazed by this GOD of Efatha. Not long ago was when my case was at it finale. I informed my Bishops husband that tomorrow is the day to go to court. I remember him telling me that, once I get into the court room, I should utter the word “EFATHA EFATHA EFATHA” and I said ok. In the morning also, I called my Bishop carol and told her that “today is my day in court”. She said to me “MAY GOD LEAD YOU. I got to court and my case began. I remember what the Bishops husband told me, to utter the word EFATHA. I started… EFATHA EFATHA” and before I got to the third, I heard the judge say that, “You Jimmy Muhando YOU ARE FREE’ you do not have a case again. Hallelujah. Immediately I ran out of the court room and the prison guards chased me, thinking that I have escaped. The people told them that he is FREE, his case has been erased. I am amazed by this GOD. And not only that, in the case about the plot; the man confessed not having any documentation on the plot and he has no claim over it. JESUS OF EFATHA IS GOOOOD! I got all these after being born again. I am amazed by this JESUS. That’s why this day I have decided to prepare this food so that I may THANK MAY GOD, I AM THANKING MY JESUS WHO WON FOR ME… that is Our GOD through JESUS HIS son."
- Get link
- X
- Other Apps
"Laana basi, Mahangaiko basi, Shauku basi, Madeni basi, Vidonda vya ndani basi na ZIMESHINDWAAAAAA.....kwa JINA LA YESU KRISTO kwa Neema na Baraka za UBABA"
- Get link
- X
- Other Apps
Mtumishi wa MUNGU Mama Eliakunda Josephat Elias Mwingira, akiwa na mtoto wa pili aliyezaliwa katika Kambi ya Viongozi 2014 Kibaha Precious, Centre, Tanzania.
- Get link
- X
- Other Apps
Aliteswa ili tuwekwe huru, Tuna kila sababu ya kuliadhimisha Jina la Yesu. JINA LIPITALO MAJINA YOTE, Alituondolea huzuni,mateso yote,mahangaiko yote, shida zote,vilio vimekoma,hakuna kuguna tena,akaichukia aibu yetu,ule uhitaji wetu, umaskini, udhaifu wetu, TUKAWEKWA HURU NA HURU KWELIKWELI, AMEN!
- Get link
- X
- Other Apps
Haleluya, MUNGU wetu MKUU ni MZURI, MUNGU wetu Anatupenda wanawe, YESU wetu ni MZURI, ROHO MTAKATIFU wetu ni MZURI... Tunamshukuru BWANA wetu YESU KRISTO Mwana wa MUNGU Aliye HAI, Kambi ya Viongozi ilikuwa nzuri sana, Baba yetu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira alitulisha Mafundisho mazuri sana yalitoka kwa BWANA wetu YESU KRISTO, Alitupatia UBABA, Alitupatia BARAKA ZA UBABA (za UTUME),... Oooh Haleluyaaaaa. YESU ANATUPENDA, Sisi ni wa mahali pa JUU, Sisi ni WAJUU, Sisi ni WASHINDIIIII, Asante YESU.
- Get link
- X
- Other Apps