DARASA/CHUMBA CHA MAFUNDISHO: ''Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY. (Darasa linaendelea lilipoishia...) "Hapa ukifuatilia utajua adui za mtu ni wa nyumbani mwake mwenyewe; wakikasirika hawa ni wabaya sana maana wanakujua vizuri na wako jirani na wewe na wanakufikia kwa urahisi; hivyo kukuharibu ni rahisi sana. Na hao wanaokuharibu ndio wenyeji! Biblia inasema utoke katika hao jamaa zako ili MUNGU awe kwako BABA. Anapozungumzia awe BABA tena BABA MWENYEZI ana maana gani?, Ana maana YEYE ATAKUTUNZA kama mtoto wake nawe utakaa kwa SALAMA bila kitu kukutikisa wala kupungukiwa na kitu. Kama Neno lisemavyo: 2 Kor 6:1-10 “Nasi tukitenda kazi pamoja naye, twawasihi msiipokee Neema ya Mungu bure kwa maana asema hivi, wakati uliokubalika nalikusikia, siku ya Wokovu nalikusudia, tazama wakati uliokubalika ndio sasa; tazama siku ya wokovu ndiyo sasa. Tusiwe kwazo la namna yoyote katika jambo lolote, ili utumishi wetu usilaumiwe bali katika kila Neno tujipatie sifa njema; kama watumishi wa Mungu, katika saburi nyingi, dhiki, misiba, shida, vifungo, fitina, taabu, kukesha, kufunga, kuwa safi, elimu, utu wema; Roho Mtakatifu, upendo, neno la kweli; nguvu za Mungu, kwa silaha za haki za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto; kwa utukufu au kwa aibu; kwa kunenewa vibaya au vema kama wadanganyao bali tu watu wa kweli; kama wasiojulikana bali wajulikanao sana! Kama wanaokufa kumbe tu hai, kama wanaorudiwa bali wasiouawa; kama wenye huzuni bali siku zote tu wenye furaha; kama maskini bali tukijitajirisha na kuwatajirisha na wengine; kama wasio na kitu bali tu wenye vitu vyote”" (Usikose darasa mwana wa MUNGU, Neema hii ni yako sasa).

Comments