DARASA/CHUMBA CHA MAFUNDISHO: ''Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY. (Darasa linaendelea lilipoishia...) Yakobo 4:6 “Lakini hutujalia sisi Neema iliyozidi, kwa hiyo husema Mungu huwapinga wajikwezao bali huwapa Neema wanyenyekevu”. Unaonaje wakati huu UJINYENYEKEZE kwa MUNGU wetu upitapo katika mambo magumu na mazito ili AKUKWEZE ili apate KUKUONYESHA njia ya kutokea na namna ya kuyashinda yanayokuzunguka. Adui wa mtu ni wa nyumbani mwake! Kagua nyumba yako sasa, jikague mwenyewe. Mfano:- Kuna Baba mmoja alisema mkewe hamfurahishi kabisa, lakini huyo mke ni wa kwako kama hajakufurahisha elewa kwamba hajafurahi. Maana hata anayesema hajashiba ni kwa sababu hajala. Tafuta kisababisho cha kumfurahisha mumeo. Katika hiyo nyumba iliyojengwa kuna wapangaji- kuna mikono, masikio, miguu, macho, n.k Lazima uangalie hiyo mikono yako imekupelekea kufanya nini? Hiyo miguu imekutembeza wapi na wapi? Ndiyo maana Biblia inasema tukae vitandani mwetu na kutulia na uitafakari sheria ya BWANA. Hebu tafakari tangu ulipozaliwa, mikono yako imefanya nini? Je umeungana na watu wasiomcha MUNGU? Je umewagawia mapato yako watu wanaokwenda kwa waganga wa kienyeji? Je hiyo miguu imekupeleka mahali pa uovu? TAFAKARI! Siyo kila sherehe unatakiwa uende; siyo kila kiti unatakiwa uweke makalio yako maana viti vingine vinawaka moto! Biblia imesema “Vikao vingine vya kifahari ni vya hila”. (Usikose Darasa, sasa ni wakati wa USHINDI)

Comments